Pages


Photobucket

Friday, November 2, 2012

MHARIRI WA BUSINESS TIMES APIGWA RISASI

Mnaku Mbani (Mhariri wa Business Times ) akiwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili leo asubuhi baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi jana akiwa anaelekea nyumbani kwake usiku wa saa mbili jioni. Katika tukio hilo alikuwa na abiria wenzake 6 ambao nao walipigwa risasi na baadhi yao kutolewa na kuruhusiwa. Mnaku alipigwa risasi juu yo mdomo na risasi hiyo kutokea kwenye shavu lake la kushoto, bado yuko chini ya uangalizi wa madaktari. 
 Kwa niaba ya Kampuni ya Business Times Limited, Bw Imma Mbuguni kupitia Blogu yake  mma Mbuguni   amesema "napenda kuwataarifu kwamba kikao cha kujadili hali na mwenendo mzima wa Mhariri mwenzetu Mnaku Mbani ndio kimekwisha na kuahidi kutoa taarifa maalum kwa vyombo vya habari ili kuelezea uhalisia wa tukio zima na nini kinaendelea kwa faida ya vyombo vyote vya habari pamoja na msimamo mzima wa Business Times Limited ,Tafadhali tunaomba uvumilivu wenu wakati tunaendelea kufuatilia taratibu zote. Asanteni na poleni"


Chanzo cha habari blog ya Imma Mbuguni 

No comments:

Post a Comment