Naibu
Waziri Mkuu wa Uingereza, Nick Clegg ameonya kwamba wabunge pinzani
katika bunge la nchi hiyo huenda wakaiona Uingereza inajitoa kwenye
Umoja wa Ulaya.
Clegg
kiongozi wa chama cha Kiliberali kinachounga mkono Umoja wa Ulaya
ameyatoa matamshi hayo baada ya Waziri Mkuu David Cameron, kushindwa
vibaya bungeni kuhusu mpango wake wa kutaka kupunguzwa kwa bajeti ya
Umoja wa Ulaya.
Cameron
amesema atapambana kuhakikisha matumizi katika bajeti yanapunguzwa.
Aidha, anataka bajeti ya muda mrefu ya Umoja wa Ulaya iongezeke sambamba
na mfumuko wa bei.
Habari hii ni kwa hisani ya idhaa ya Kiswahili ya DW.
No comments:
Post a Comment