Pages


Photobucket

Monday, November 5, 2012

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Yupo Nchini Ujerumani Kwa Matibabu

 Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa
--
ALIYEKUWA Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne, Edward Lowassa yupo nchini Ujerumani kwa matibabu na uchunguzi wa kiafya.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli jana hakuwapo katika uzinduzi wa mradi wa Barabara ya Minjingu hadi Arusha na shule jimboni kwake, uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete aliye ziarani mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Jowika Kasunga na baadaye kusambazwa kwa waandishi wa habari, Lowassa alieleza kusikitishwa kutokuwapo jimboni kwake wakati huo ambao Rais Kikwete anatembelea jimbo lake.

Lowassa alisema kuwa, hali hiyo imetokana na kuwa safarini kwa ajili matibabu lakini akasema anaamini mambo yataenda vizuri si kwa ziara hiyo ya Rais Kikwete bali hata vikao vya juu vya CCM vinavyotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Katika taarifa hiyo, alimsifu  Rais Kikwete kuwa, kutokana na kutekeleza vizuri na kwa uadilifu Ilani za uchaguzi za CCM, wiki mbili zijazo wanaCCM watakwenda Dodoma kuidhihirishia dunia  na Watanzania wenye shaka kwamba wanamwamini na kuuthamini uongozi wake.

Katika maelezo hayo, Lowassa alieleza tatizo linalomsumbua kuwa ni macho, lakini pia atatumia nafasi hiyo kuchunguza afya yake.

No comments:

Post a Comment