Na Bosire Boniface, Wajir
Al-Shabaab inajaribu kupata nguvu ya msaada wa kimataifa kwa wapiganaji
wake waliokata tamaa baada ya kupoteza ngome ya mji wa bandari wa
Kismayu kwa kutoa vitisho kwa nchi kadhaa, maofisa wa usalama na
wachambuzi wasema.
Mwanaume akitia rangi ya kufuta alama ya
al-Shabaab huko Wanlaweyn tarehe 11 Oktoba baada ya vikosi vya Umoja wa
Afrika na vya serikali kukamata mji huo kutoka kwa kikundi hicho cha
wanamgambo. [Mohamed Abdiwahab/AFP]Al-Shabaab imekuwa ikihuisha akaunti
yao ya Twitter mara kwa mara kutoka ilipopoteza katika jaribio la
kubakia kuwa muhimu na kushawishi wafuasi wake kujilinda dhidi ya kile
inachokiita vita na ukatili dhidi ya Waislamu wasio na hatia.
Kikundi hicho cha wanamgambo kimetishia kushambulia Uingereza pamoja na nchi jirani na Somalia.
Katika mfululizo wa matangazo 15 yaliyotolewa kwenye mtandao wa Twitter
tarehe 22 Oktoba, al-Shabaab ilisema kuwa Uingereza "itagharimia sana
jukumu lake la kutokuwa na haya katika vita dhidi ya Uislamu na ukatili
usiokwisha dhidi ya Waislamu wasio na hatia".
"Jinamizi ambalo kwa siri lilionekana kuwa tishio kubwa kwenye fuko za
Uingereza lilikwenda mpaka kusababisha vitisho vilivyounganishwa vya 7/7
na 21/7," al-Shabaab ilisema.
Mabomu yaliyopiga London tarehe 7Julai, mwaka 2005, yalikuwa mfululizo
wa mashambulio ya kujitoa muhanga yaliyoratibiwa kwenye mfumo wa usafiri
wa umma wa jiji hilo ambayo yaliwaua raia 52 na walipuaji wanne. Wiki
mbili baadaye, mashambulio manne yalijaribu kuharibu sehemu ya mfumo wa
usafiri wa umma wa jiji hilo.
Al-Shabaab pia iliapa kulipiza kisasi kwa uamuzi wa Mahakama Kuu ya
London kumrejesha mwalimu wa dini ya Kiislamu mwenye msimamo mkali
Mustafa Kamel Mustafa, ambaye anajulikana sana kama Abu Hamza al-Masri,
kwenda Marekani tarehe 5 Oktoba kuhukumiwa katika nchi aliyofanya kosa.
Mustafa alishtakiwa kwa kuweka kambi ya mafunzo huko Oregon, kosa ambalo
alilikana tarehe 9 Oktoba katika mahakama ya New York
Siku ya Jumapili (tarehe 28 Oktoba), kikundi hicho cha wanamgambo hao
ilirudia tena vitisho dhidi ya Kenya , ambayo jeshi lake limekuwa
likipigana na al-Shabaab nchini Somalia kwa kipindi cha zaidi ya mwaka.
"Maadui tunaokumbana nao wamefanya ukokotozi mbaya wa kihistoria wakati
walipotuma Kenya kuvamia ardhi ya Kiislamu ya Somalia," alisema mmoja wa
wasemaji wake anayedhaniwa kuwa kiongozi wa al-Shabaab Mukhtar Abu
Zubayr, pia anayejulikana kama Ahmed Godane. "Kenya hivi punde itajuta
kwa kujiingiza kwake katika jambo hili, Insha Allaah [Mungu akipenda]."
Vitisho ni mwito wa kukusanya nguvu ya kuongeza hamasa
Wachambuzi na viongozi wa usalama waliiambia Sabahi kwamba vitisho
vinafanywa na kundi lililofungamana na al-Qaeda ili kubadili mwelekeo
kutokana na kuipoteza Kismayo.
Mwanajeshi mstaafu Meja Bashir Hajji Abdullahi, mchambuzi na mshauri wa
usalama anayeishi Nairobi, alisema uongozi wa kundi hilo una matumaini
ya vitisho hivyo kuifikia operesheni ya nchi za ugenini ambayo
haitawawafanya al-Shabaab wahusike tu kimataifa, lakini pia kuwashangaza
wapiganaji wake ambao alisema wanajisikia kushushwa hadhi baada ya
kupotoshwa kufikiria kwamba walikuwa wasioshindika huko Kismayo.
David Ochami, mwandishi wa habari anayeishi Mombasa ambaye anayefuatilia
wanamgambo huko Mashariki ya Kati na Pembe ya Afrika wa gazeti la The
Standard la Kenya, aliiambia Sabahi kwamba vitisho vya al-Shabaab
visidharauliwe kutokana na upotevu wa hivi karibuni.
"Kwa kuwa na wanajihadi wageni katika ngazi zake, hata mwanamgambo moja
ni hatari," alisema Ochami. "Wanaweza kukosa eneo ambalo watalitumia
kuunda, lakini watajipanga sana katika mbinu za vita vya msituni ili
waendelee kuwepo."
Tishio linaweza kuonekana kama mwito wa kukusanya nguvu kwa ajili ya
kuongeza hamasa ya wapiganaji wa al-Shabaab ambao wametoroka na kuungana
na wananchi wengine, kwa mujibu wa Ochami.
Alisema vitisho vya al-Shabaab dhidi ya Uingereza haitomaanisha
kushambulia ardhi ya Uingereza, aliongeza kwamba uangalifu mkubwa
unahitajika kuilinda Uingereza na nchi nyingine za kigeni huko Kenya na
sehemu nyingine.
Bado, Ochami aliudharau uwezo wa al-Shabaab kufanya shambulio kubwa, hata karibu na nyumbani.
"Hakuna anayepoteza usingizi siku hizi wanapotoa vitisho kwa sababu
hawana uwezo wa kufanya shambulio la hali ya juu kwa muda mfupi,"
alisema.
Waziri wa Ulinzi wa Kenya Yusuf Haji alisema serikali inavizingatia
vitisho hivyo na inawasiliana na balozi za nchi za nje kila siku
kuangalia vitisho hivyo na kutafuta njia gani nzuri za kukabiliana
navyo.
"Tupo tayari kwa vita na wanamgambo," aliiambia Sabahi. "Itakuwa ndefu, lakini uzuri wakati wote hushinda ubaya."
No comments:
Post a Comment