Wizara ya Mashauri ya Nchi za 
Nje ya Uingereza imeonya kwamba uwezekano unazidi kwamba kutatokea 
mashambulio ya kigaidi katika eneo la Sinai nchini Misri; na imezidisha 
uzito wa onyo hilo kutoka la kawaida na kuwa kubwa zaidi.
Ilani hiyo imetolewa kutokana na taarifa za hivi
 karibuni kuhusu ile inayosemekana kuwa njama ya al-Qaeda na kupatikana 
kwa silaha katika eneo hilo la Sinai.
Piya linafuata polisi wa Misri kugundua kikundi 
cha magaidi mjini Cairo, na baadhi ya taarifa zinaeleza magaidi hao 
wakipanga kushambulia watalii kutoka mataifa ya Magharibi.
Hata hivyo Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya 
Uingereza inasema hali katika maeneo ya watalii ya Bahari ya Sham, 
pamoja na Sharm el Sheikh, ni tulivu.
CHANZO NA BBC
 
 


No comments:
Post a Comment