Pages


Photobucket

Friday, November 9, 2012

RIPOTI YA NGWILIZI YASOMWA BUNGENI, WATUHUMIWA WOTE WASAFISHWA



Brigedia general Hassan Ngilizi mwenekiti aliyekuwa anaongoza uchunguzi..
Spika wa Bunge Anna Makinda  Wakati akisoma taarifa hiyo leo Bungeni Mjini Dodoma..
Mh sara Msafiri aliyekuwa anatuhumiwa.Amekutwa hana hatia katika ripoti hiyo..
Mh Maswi Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Amepewa Onyo kali  na spika wa Bunge la tanzania..
Waziri wa Nishati na Madini Mh Profesa Sospeter Muhongo nayea ameagizwa kuwa muangalifu katika hotuba zake kwa kuwa ni muwakilishi wa serikali..
Mh Tundu Lisu ambaye aliongea na waandishi wa habari na kuwatuhumu baadhi ya bunge naye amepewa onyo kali na spika wa bunge la tanzania..
Mheshimiwa John Mnyika mbunge wa ubungo na msemaji wa kambi ya upinzani bungeni ambaye nae katika hotuba yake aliwatuhumu baadhi ya wabunge nae amepewa onyo kali..
Mh selasini mbunge wa Rombo nae alisimama bungeni wakati akichangia hoja ya bugeti ya nishati na madina nae amepewa onyo kali na spika wa bunge la tanzania..
 
Sehemu ya taarifa hiyo...

Maswi aliwatuhumu moja kwa moja baadhi ya wabunge kwa maandishi kutaka rushwa na wakimtishia kupoteza nafasi yake ya Ukatibu wa Wizara
- Tume inasema Maswi alitoa tuhuma hizi kwa lengo la kujihami juu ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili
- Tuhuma za kuwa Maswi aliombwa rushwa ya Milioni 50 na wabunge nazo zimetupiliwa mbali kuwa lengo ni kutaka kujihami.
- Mbunge Selasini alipohojiwa na Tume, alikiri kuwa hakuwa na ushahidi wa maneno 'aliyoropoka' bungeni akiwatuhumu baadhi ya wabunge waliohisiwa kupokea rushwa.
- Mnyika alipohojiwa juu ya kauli yake Bungeni kuwa Maswi anashinikizwa ajiuzulu nafasi yake, Mnyikaalitumia ushahidi wa vyombo mbalimbali vya habari! Anadai kuwa hakukuwa na kanusho la habari hizo (labda ndilo lilimpelekea kuamini ni habari sahihi)
- Ole Sendeka alipohojiwa juu ya kauli yake bungeni; alidai kuwa alikuwa anajaribu ku pre-empty tu.
- Mbunge Kessy naye alijikanyaga tu kuwa lazima kulikuwa na rushwa tu
- Waziri Muhongo alipohojiwa na Tume alisema ni 'allegations' tu.
- Mbunge Sarah Msafiri na mwenzake wamesafishwa, hawakuiuzia TANESCO matairi! Tuhuma za Tundu Lissu pia zimeonekana kukosa mashiko na amekiri kuwa alipata taarifa toka kwa watu wa Wizara, hakuwa na ushahidi wa moja kwa moja!
- Wabunge waliotoa tuhuma bungeni, wamekemewa na kutakiwa kutorudia tena.
- Lissu amekaripiwa vikali kwa kuwachafua wabunge na waliochafuliwa wameombwa wamsamehe bure.
- Waziri Sospeter Muhongo amekaripiwa kwa kuwachafua wabunge na ametakiwa awe mwangalifu anapotoa kauli yoyote bungeni kwakuwa kauli yake inachukuliwa ni kauli ya Serikali.

No comments:

Post a Comment