Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad
akisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo
Said Ali Mbarouk (mwenye fulana), kuhusiana na kubomoka kwa jengo la
makumbusho kuu ya Zanzibar-Picha na Salmin Said-Ofisi Ya Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar
--
Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameuagiza uongozi wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kuzuia matumizi ya jengo la
Makumbusho kuu ya Zanzibar baada ya kupata athari za kubomoka juzi
usiku.
Maalim Seif ametoa agizo hilo
baada ya kutembelea na kuangalia maharibiko yaliyotokea baada ya jengo
hilo kubomoka sehemu ya upande wa Ngome Kongwe na kusababisha hasara
kubwa.
Hata hivyo Makamu wa Kwanza wa
Rais ameelezea haja ya kulifanyia matengenezo jengo hilo ili kutunza
historia ya Zanzibar na hifadhi ya Mji Mkongwe ambao ni urithi wa
Kimataifa.
Akizungumzia hali hiyo, Waziri wa
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Said Ali Mbarouk
amesema jengo hilo limepata athari hiyo wakati likiendelea kufanyiwa
ukarabati.
Amesema baada ya kuona athari
zilizojitokeza hapo kabla, waliamua kulifanyia ukarabati kwa kuanza na
hatua ya uezekaji, lakini mvua zinazoendelea kunyesha zimekuwa
zikipelekea jengo hilo liendee kuvuja na kupelekea kubomoka sehemu
hiyo.
Amesema kutokana na athari hiyo, wameamua kuitisha kikao ili kutathmini hasara iliyopatikana na kutokana na uharibifu huo.
Mhe. Mbarouk amefahamisha kuwa
baada ya kikao hicho watashauriana na washirika wa maendeleo wakiwemo
mradi wa MACEMP uliokuwa ukisaidia kulifanyia ukarabati jengo hilo
pamoja na majengo mengine ya kihistoria, ili waweze kuendeleza ukarabati
huo.
Jengo la Makumbusho kuu la
Zanzibar ni miongoni mwa majengo muhimu sana ya kihistoria ambapo
inasemekana hata umeme ulianza kuwaka katika kituo hicho katika eneo
zima la Afrika Mashariki.
Na
Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment