Kufuatia kupigwa risasi, kujeruhiwa begani na kulazwa
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa mwandishi wa Tanzania Daima
Bwana Shabani Matutu (30) ambaye pia ni mwanachama hai wa Dar City
Press Club(DCPC), uongozi wa Klabu uliamua kufuatilia tukio hilo kwa
karibu ili kujua na kuhakiki kwa kina yaliyotokea na sababu
zilizopelekea
hayo kutokea.
hayo kutokea.
Kutokana na hayo DCPC imebaini yafuatayo:-
1. Ni kweli kwamba Shabaan matutu(30) alipigwa risasi na
askari wa jeshi la Polisi mwenye namba F.8991 D/C Idrissa nyumbani
kwa Shabaan kimakosa baada ya askari huyo na wenzake wanne kufungua
kwa nguvu na bila ya kujitambulisha kwa mwenye nyumba (Shabaan na
Mkewe) licha ya kuombwa kufanya hivyo kabla.
2. Kuna maelezo yanayokinzana katika kuelezea jinsi tukio
hilo lilivyotokea kwa pande mbili zinazohusika yaani maelezo ya shabaan
na ya polisi
3. Kwamba sababu za askari polisi hao kufanya hivyo
hazikuwa zimefanyiwa uchunguzi wa kutosha hadi kujiridhisha kuchukua
hatua hiyo hivyo hata wao walikiri kukosea pamoja na kueleza kwamba
Shabaan ndiye aliyeaanza kuwashambulia askari Polisi kabla ya wao
kumjeruhi kwa risasi.
4. Shabaan mpaka sasa anaendelea na matibabu licha ya
kuuguza majeraha aliyosababishiwa na polisi na kwamba ameshauriwa
kitaalamu kupumzika nay eye binafsi ameomba asibughudhiwe ili afya yake
irejee haraka na kwamba pindi atakapokuwa katika hali nzuri zaidi ya
sasa kwa mujibu wa ushauri huo wa kitabibu, atawasiliana na yeyote
wakiwemo polisi ambao wamekuwa wakimmghasi kwa kuja kumhoji mara kwa
mara.
Kwa sababu hizo basi Dar es Salaam City Press Club:-
Kwa sababu hizo basi Dar es Salaam City Press Club:-
1. Tunaiomba Serikali na mamlaka za juu zaidi ya jeshi la
Polisi hususan Wizara ya mambo ya ndani ifanye uchunguzi wa kina na
huru wenye kuhusisha taasisi wakilishi katika jamii juu ya tukio hilo
na kulichunguza jeshi la polisi linavyofanya kazi zake kwa
kuzingatia kanuni na sheria.
2. Tunalitaka Jeshi la Polisi liache mara moja kutuma askari
wake kwenda kwa Shabaan kwa lengo la kumhoji ama kutaka atoe maelezo
yake kwa viongozi wa jeshi hilo ilhari walishamtuhumu na kueleza
kuwa aliwashambulia Polisi kwa Panga kabla ya wao kumfyatulia
risasi. Tunasema hivi kwa kuzingatia kanuni za afya na haki za msingi
za binadamu.
3. Tunalitaka Jeshi la Polisi liueleze umma bila kuficha
ukweli na kwa jinsi ile ile ambayo lilitoa taarifa mara baada ya
tukio, lieleze kwa nini linatumia habari na vyanzo dhanifu kujeruhi
na kuhatarisha maisha ya raia wasio na kosa huku likitoa
maelezo yasiyofanyiwa uchunguzi.
4. Mwisho tunalitaka jeshi la Polisi lenyewe lijitafiti
na kujipanga upya ili liweze kufanya kazi kisayansi na weledi
kama ambavyo viongozi wake wamekuwa wakijinadi mbele ya vyombo vya
habari.
Tamko hili limetolewa leo Tarehe 08/Desemba/2012.
Joseph Kayinga
Katibu Mkuu-DCPC
Source: wavuti.com
No comments:
Post a Comment