Rais wa Madagascar, Mheshimiwa Andry Rajoelina ambaye amewasili
mjini Dar es Salaam mchana jana Ijumaa, Desemba 14 kwa ziara ya kikazi ya
siku mbili nchini akiwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu, tayari kuanza mazungumzo rasmi.
Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa Tume ya Siasa, Ulinzi
na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo amepewa jukumu na
viongozi wenzake ndani ya Jumuiya hiyo kukutana na viongozi wa Madagascar kuwaelezea
maamuzi ya mkutano wa viongozi hao wa SADC uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini
Dar Es Salaam.Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu, Dar
Es Salaam, mwanzoni mwa wiki hii, Mheshimiwa Ravalomanana alithibitisha kuwa
amekubaliana na maamuzi ya viongozi wa SADC.
Miongoni mwa mambo mengine, viongozi hao wa SADC wanataka
viongozi hao wawili wa Madagascar washawishiwe na wakubali kutogombea katika
Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwakani.
No comments:
Post a Comment