Shirilisho la Ngumi la Kimataifa (IBF)
limepongeza bingwa mpya wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika,
Ghuba ya Uajemi na Mashariki yaa Kati, Mtanzania Francis Cheka.
Katika barua yake aliyomtumia Francis Cheka ya tarehe 28/12/2012
Mwenyekiti wa kamati ya Ubingwa wa IBF/USBA Lindsey Tucker alisema
“Tunachukua fursa hii kukutakia maisha na mafanikio mazuri kama bingwa
wa IBF na kumhimiza kuishi kama bingwa”. Cheka atatakiwa kutetea taji
lake katika kipindi cha miezi sita kufikia mwezi wa 6 mwakani dhidi ya
mpinzani ambaye ana rekodi ya mapambano yasiyopungua 15 na mengi awe
ameyashinda hususan mapambano mawili ya mwisho
No comments:
Post a Comment