Tanzania
Bunge Sports Club Football imefanya maajabu katika uwanja wa Nyayo
jijini Nairobi jana kwa kuwabamizwa wenyeji wao timu ya Kenya Bunge
Sports Club Football mabao 5 kwa nunge katika michezo ya mabunge ya nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini Nairobi. Mashindano
hayo yaliyofunguliwa rasmi juzi tarehe 7 Disemba na Spika wa Bunge la
Afrika Mashariki Mh. Margreth Natongo Zziwa akisisitiza “let the best
team win” tayari yamezikutanisha timu ya Bunge la Uganda na timu ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo timu hizo zimetoka sare ya 1-1.
Wakati
wa kuhitimisha karamu ya mabao kwa timu ya Kenya, Watanzania walijikuta
uwanjani peke yao wakishangilia huku mashabiki-wenyeji wakiwa
wameondoka uwanjani hapo.
Leo Tanzania itapambana na Rwanda kwenye mpira
wa miguu katika uwanja wa City Stadium, na Wabunge wanawake watakutana
na Kenya kwenye mpira wa kikapu Nyayo Stadium. Mashindano haya
yanalenga kuimarisha ushirikiano na kuitangaza zaidi Jum uiya ya Afrika
Mashariki.
Katika
mashindano haya ambayo hufanyika kila mwaka huyakutanisha mabunge ya
nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda. Waratibu wa michezo
hii ni Jumuiya pamoja na Bunge la Afrika Mashariki. Kwa mwaka huu
Burundi haikushiriki.
Chini
ya ukufunzi wa Naibu Waziri (TAMISEMI) Mhe. Kasim Majaliwa (Mb) .na
uongozi wa Mhe. Idd Azzan (Mb) mabao hayo yalifungwa na Mhe Amos Makala
(Mb), Yusuf Soka (2), Mark Tanda na Mhe. Joshua Nassari.
(Na Prosper
Minja).
No comments:
Post a Comment