Na: Ali Issa Maelezo Zanzibar
Waziri wa Habari Utamaduni, utalii na
Michezo Zanzíbar Saidi Ali Mbaruok amesema wakati umefika sasa kwa
wandishi wa habari wa Zanzíbar kupata nafasi ya kwenda nchi za nje kuitangaza
Zanzíbar kiutalii kila itapo fanyika Maonyesho, makongamano na mikutano ya
utalii duniani.
Hayo ameyasema leo huko Ofisini kwake
Wizara ya Habari Utamaduni, Utalii na Michezo kikwajuni
wakati alipo kutana na wajumbe wa Bodi ya ushauri wa magazeti na majarida
walio fika ofisini kwake kwa kujitambulisha.
Amesema kua ni vyema kwa waandishi wa
habari kwenda kuandika habari zinazi huso utalii na zaidi pale Zanzíbar inapo
shiriki katika maonesho ya kimataifa nyanayo mfanyika katika nchi mbalimbali ili
kuutangaza utalii wake .
“Wandishi kupata frusa hii ya kwenda nje
kuitangaza Zanzíbar kiutalii ni jambo zuri na
linalo kubalika kwani tume shuhudia kuona wandishi wahabari
kutoka nchi mbali mbali duniani wana tangaza nchizao na sioni haja kwanini sisi
tusifanye hivyo kwani asilimia kubwa za fedha za kigeni za Zanzíbar hupatikana
kwajia hiyo.
Alisema kuwa wandishi ni hakiyao kwenda na
hakuna sababu kua wasende kwani watacho kifanya wao ni maendeleo ya taifa lao
kijumla na wataweza kuitangaza Zanzíbar kwa njia pana na kuweza kueleweka zaidi
utalii na hatimae kufaidika.
Nae Mwenyekiti wa Bodi hiyo ambae pia ni
Mshauri wa Rais wa masuala ya utalii Issa Ahmed Othuman mapema akimkaribisha
waziri alisema kua maonyesho ya utalii yajayo kuazia ni vizuri kwa
mwandishi wa Habari akawemo katika katika msafara utakao
shiriki katika maonesho yatakayo katika nchi yoyte Duniani.
“Naahidi waandishi wahabari watakuwemo kila
safari kwa kuitangaza Zanzíbar kiutalii na nitaazia safari ya ujerumani”.alisema
Issa Ahamed.
Aidha mwenyekiti huyo alima kua atakuwa
pamoja na waziri kuona kua bajeti maalumu inawekwa ilikuhakikisha kua wandishi
wanapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika maonesho yote ya utalii yanayo
fanyika ndani na nje ya nchi kwa miajili ya kuitangaza zaidi Zanzíbar kiutalii.
Wakati huo huo waziri wa habari Utamaduni
,Utalii na Michezo Said Ali Mbaruok amezindua Bodi ya Tume ya Utangazaji
Zanzíbar huko katika Ofisi za Tume ziliopo kikwajuni Zanzíbar
.
Waziri ameitaka bodi hiyo kuwa makini
katika kusajili vyombo vya redio na Televisheni kwa mustakbali wakuwa na vyombo
bora vyenyekuelimisha jamii na kuondokana na vyombo vitakavyo leta mfarakano
nchini .
Bodi hiyo ipo chini ya Mwenyekiti wake
Abdalla Mwinyi Khamis ambae pia Mkuu wa Mkoa Mjini Maghari Unguja
iliteuliwa hivi karibuni ambapo Rais wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi alimteua Mwenyekiti na wajumbe kuteuliwa na Waziri.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO
ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment