Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia
Stella Manyanya akihutubia wananchi wa kata ya Matanga leo katika ziara
yake ya siku 8 kwa ajili ya kuhamasisha shughuli za kilimo Mkoani Rukwa.
Ziara hiyo itahusisha Wilaya zote tatu za Mkoa wa Rukwa ambazo ni
Sumbawanga, Kalambo na Nkasi pamoja na
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipokea maelezo ya shamba
darasa kutoka Afisa Ugani Kata ya Matanga Ndugu Edith Shirima leo
alipoanza ziara yake Mkoani Rukwa kwa kuanzia katika kata hiyo. Kulia ni
Afisa kilimo Manispaa ya Sumbawanga Ndugu George Lupilya, Kaimu Katibu
Tawala Wilaya ya Sumbawanga. Kushoto ni Katibu wa Mkuu huyo Mkoa Frank
Mateni.
Shamba
darasa katika kata ya Matanga kijiji cha matanga linalomilikiwa na
Mkulima mdogo Bibi Paschalia Ntinda. Mbolea ya kupandia iliyotumika ni
Minjingu Mazao.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akisalimiana na Bibi Paschalia Ntinda amabaye ni mmiliki wa shamba darasa hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kushoto akisalimiana na
wananchi wakulima katika kata ya kasense leo alipoenda kukagua mashamba
darasa katika kata hiyo. Kata ya Kasense ipo katika Manispaa ya
Sumbawanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kulia akishiri katika palizi
ya mahindi na kinamama wakulima wa kata ya Kasense leo akiwa ziarani
katika kata hiyo kwa ajili ya kuhamasisha shughuli za kilimo Mkoani
Rukwa.
Ziara
hii ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa inaenda sambamba na chanjo ya minyoo na
vitamin A kwa watoto walio chini ya miaka mitano. Kwa kuunganisha zoezi
hili na ziara yake kunatoa fursa kubwa kwa wananchi hususani wa vijijini
kuwafikisha watoto wao kupata chanjo hizo kwa wingi na kirahisi. Katika
kata ya Matanga yenye vijiji vitatu jumla ya watoto 86 walipatiwa
chanjo hiyo.
Halmashauri zake. Ziara yake inabeba ujumbe huu ufuatao:
1. Mkuu
wa mkoa wa Rukwa anawatakia kila la kheri wananchi wote katika
kusherekea sikukuu ya Noeli na Mwaka Mpya. Anawaomba kudumisha amani,
Upendo na Mshikamano kwenye maeneo yetu na tupashane habari. Toa taarifa
Polisi kwa jambo lolote lisilo la kawaida. Tuwatambue wageni wote
wanaofika katika maeneo yetu wengine si watu wema.
2. Mkuu wa mkoa anawataka viongozi wote katika ngazi zote kuwajibika na kuwa waadilifu katika kutimiza wajibu wao.
3. Kila
familia ihakikishe kuwa inatumia fursa hii ya msimu wa mvua katika
kujiondoa na balaa la njaa na pia umaskini wa kipato. Viongozi wa kata
na vijiji wafuatilie ili kujua kila kaya imelima kiasi gani katika msimu
huu. Kila kijiji kiwe na Daftari la wakulima. Wakulima
watashindanishwa.
4. Kila
kijiji kitenge maeneo maalum kwa ajili ya kuendeleza shughuli maalum
kama Ufugaji, kilimo na kuchague nguzo yake kuu ya uchumi. (Mpango wa
SAGCOT).
5. Watoto
wote watakaofaulumwaka huu wa 2012 lazima wapelekwe shule. Watoto wa
kike wanastahili kulindwa ili wasipate ujauzito. Mzazi awe mlinzi namba
moja.
6. Akina mama wapeleke watoto wao wa chini ya miaka mitano ili kupata chanjo ya minyoo na Vitamin A.
7. Kuanzia
mwezi wa Januari 2013 watoto wa miezi 9 watapatiwa chanjo ya kuzuia
kuharisha na Kichomi. Hivyo wazazi wote tuwapeleke watoto kupata chanjo
hiyo. Malengo yetu ni kuwapa chanjo watoto wote.
8. Lishe bora ni muhimu kwa familia. Kula samaki mboga mayai, wanga na nyama kadiri inavyowezekana.
9. Nawashukuru kwa jinsi mnavyoniunga mkono, nami nawapenda sana.
Na, Lukaza BLOG
No comments:
Post a Comment