Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize
|
Na Sabina Chrispine Nabigambo
Marekani imeondoa ubalozi wake katika nchi ya Jamhuri ya Kati wakati huu
ambapo kiongozi wa taifa hilo ameomba msaada wa kijeshi kwa Ufaransa na
Marekani baada ya waasi kudhibiti miji kadhaa nchini humo.
Jana Marekani ilisema kuwa imeondoa mabalozi wake nchini humo na
kusitisha utendaji wake kwa muda na kwamba haijavunja uhusiano wa
kidiplomasia na serikali ya nchi hiyo ingawa imewaonya raia wake
kutosafiri kuelekea nchini humo wakati huu machafuko yakiendelea.
Umoja wa mataifa pia umeanza kuwaondoa wafanyakazi wake huku wapiganaji
waasi wamepiga hatua kuingia katika mji mkuu Bangui na kuamsha hofu kwa
wakazi wa mji huo.
Aidha rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa nchi yake
haitatumia vikosi vyake kuingilia mzozo unaoendelea nchini Jamhuri ya
Afrika ya Kati huku akisisitiza kuwa uwepo wao nchini humo si kwa lengo
la kulinda serikali bali kulinda na kutetea maslahi yao.
Rais Francois Bozize ameomba mataifa yenye nguvu ikiwa ni pamoja na
Ufaransa na Marekani kuisadia kijeshi ili kudhibiti waasi wanaoendelea
kupig a hatua kuingia mji wa Bangui huku akitaka pia msaada wa
kufanikisha mazungumzo ya kutatua mzozo huo mjini Libreville.
Chanzo-kiswahili.rfi.fr
Chanzo-kiswahili.rfi.fr
No comments:
Post a Comment