Mjumbe
maalumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Suzan Rice ambaye pia ni
mtu wa karibu wa Rais Barack Obama wa Marekani amejitoa katika orodha ya
watu wanaotazamiwa kuchukua nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi
hiyo.
Bi. Rice amekuwa akikabiliwa na shutuma kali kutoka kwa wafuasi wa chama
cha Republican kutokana na kauli aliyoitoa baada ya kutokea kwa
mashambulizi dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi, Libya
tarehe 11 Septemba mwaka huu ambayo yalisababisha vifo vya maafisa wanne
akiwemo Balozi Chris Stevens.
Katika barua aliyomuandikia Rais Obama, Bi. Rice amemweleza kiongozi
huyo kuwa anathamini heshima aliyopewa ya kuwa mmoja wa watu
wanaotazamiwa kushika nafasi ya waziri wa mambo ya nje, lakini akasema
kuwa anaamini kama atateuliwa, hatua hiyo inaweza kuambatana na
mtafaruku wa kisiasa.
Chanzo: dewjiblog.com
No comments:
Post a Comment