Na Veronica Kazimoto – MAELEZO
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amefanikiwa
kufanya mazungumzo na Rais wa zamani wa Madagaska Marc Ravalomanana
ambaye amekubari kurudi nchini kwake baada ya kuwa uhamishoni nchini
Afrika Kusini tangu mwaka 2009.
Rais wa zamani wa Madagascar Marc
Ravalomanana akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari
Ikulu jijini Dar es salaam leo December 11, 2012,kulia ni Mwenyeji wake
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam
leo, Raisi Kikwete amesema Ravalomanana amekubali pia kutokugombea
katika uchanguzi utakaofanyika nchini humo mwezi Mei 2013 ili kuleta
amani na utulivu.
“Nimezungumza na Rais Ravalomanana na amekubali kurudi nchini kwake
madagaska na kukubali kutokukugombea uchaguzi ujao kama maamuzi ya
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) yalivyofikiwa
katika vikao vyake vya hivi karibuni”, amesisitiza Rais Kikwete.
Raisi kikwete amefafanua kuwa Ravalomanana anarudi nchini Madagaska
bila masharti yoyote na atapewa ulizi na Serikali ya nchi hiyo
ikisaidiana na Jumuiya ya SADC. Kwa upande wake Rais Ravalomanana
amemshukuru Rais kikwete kwa kufanikisha mazungumzo hayo na amesema
anaheshimu maamuzi yaliyotolewa na SADC kwa lengo la kuisaidia Madagaska
kuwa katika hali ya amani.
“Ninamshukuru Rais Kikwete kwa kufanikisha mazungumzo haya na niko
tayari kurudi nchini kwangu kujenga, kuimarisha na kushirikiana na
wananachi ili kuleta amani na utulivu,” amesema Ravalomanana.
Rais kikwete alipewa jukumu na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini
mwa Afrika la kufanya mazungumzo na Marais wote wa wawili, Rais wa
sasa wa Madagaska Andry Rajoelina na Rais wa zamani Marc Ravalomanana
ambapo mazungumzo bado yanaendelea kwa upande wa Rais Rajoelina.ezi Mei
2013 ili kuleta amani na utulivu.
“Nimezungumza na Rais Ravalomanana na amekubali kurudi nchini kwake
madagaska na kukubali kutokukugombea uchaguzi ujao kama maamuzi ya
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) yalivyofikiwa
katika vikao vyake vya hivi karibuni”, amesisitiza Rais Kikwete.
Raisi kikwete amefafanua kuwa Ravalomanana anarudi nchini Madagaska
bila masharti yoyote na atapewa ulizi na Serikali ya nchi hiyo
ikisaidiana na Jumuiya ya SADC. Kwa upande wake Rais Ravalomanana
amemshukuru Rais kikwete kwa kufanikisha mazungumzo hayo na amesema
anaheshimu maamuzi yaliyotolewa na SADC kwa lengo la kuisaidia Madagaska
kuwa katika hali ya amani.
“Ninamshukuru Rais Kikwete kwa kufanikisha mazungumzo haya na niko
tayari kurudi nchini kwangu kujenga, kuimarisha na kushirikiana na
wananachi ili kuleta amani na utulivu,” amesema Ravalomanana.
Rais kikwete alipewa jukumu na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini
mwa Afrika la kufanya mazungumzo na Marais wote wa wawili, Rais wa
sasa wa Madagaska Andry Rajoelina na Rais wa zamani Marc Ravalomanana
ambapo mazungumzo bado yanaendelea kwa upande wa Rais Rajoelina.
Chanzo: mrokim.blogspot.com
No comments:
Post a Comment