GARI
AINA YA SCANIA LENYE CABIN NA. T 840 BST LIKIWA NA TRAILER NAMBA T 566
BNQ LILIGONGWA KWA NYUMA NA TOYOTA RAV 4 T 770 BMP HUKO TANANGOZI
IRINGA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WA TANO WA FAMILIA MOJA PAPO HAPO
WALIOKUWA KATIKA GARI HILO RAV 4
Na Francis Godwin
Ajali
mbaya imetokea mkoani Iringa jana mchana na kusababisha vifo
vya watu wanne wa familia moja pamoja na mfanyakazi wa ndani.
Ajali
hiyo imetokea katika eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa kwenye
kizuizi cha barabara cha mafundi wa kutengeneza barabara kuu ya Iringa
-Mafinga mkoani Iringa mida ya saa nane mchana
Kwa
mujibu wa mashuda wa tukio hilo chanzo cha ajali hiyo ni dereva
wa gari dogo aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BMP
kulipalamia lori lenye tela kwa nyuma. Huku
chanzo kikitajwa kuwa ni kuendesha kwa mwendo kasi wa dereva wa
gari ndogo marehemu Ezekiel Mwaiteleke na kushindwa kulimudu na
kulipalamia lori kwa nyuma.
Kwa mujibu wa mashuda wa tukio
hilo chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4
kuendesha kwa mwendo kasi na kushindwa kulimudu na kulipalamia lori
kwa nyuma na kuwa gari hiyo ilikuwa ikitokea jijini Dar es Salaam
kwenda Kyela mkoani Mbeya.
Hivyo
katika ajali hiyo abiria wote wanne akiwemo baba na mama wa
watoto wawili waliokuwemo katika gari hiyo pamoja na watoto hao
kufa papo hapo na maiti zote kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa
Iringa.
Majina ya waliokufa ni pamoja na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni dereva wa gari hilo na baba wa familia hiyo ,mkewe Grace Mwaiteleke ,mtoto Kelvin Mwaiteleke (2),Happy Mwandike na mfanyakazi wao wa ndani aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel huku majeruhi katika ajali hiyo ni mmoja na amekimbizwa Hospital ya mkoa wa Iringa.
WWW.FRANCISGODWIN.BLOGSPOT.COM
No comments:
Post a Comment