Na: Rodrick
Maro
Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na mashirika mengine,
yamefanikiwa kufanya maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, miaka 64 ya
Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu, la mwaka 1948 na Kilele cha Siku 16 za
Kupinga Ukatili wa Jinsia.
Mambo
mbalimbali yalifanyika, ikiwa ni pamoja na maandamano, mawasilisho ya hotuba
mbalimbali na burudani kutoka kwa vikundi mbalimbali vikiwemo Jakaya Arts
Theatre, Dancers wa Kibasila Secondary, Maigizo Human Rights Clubs kutoka Vyuo
vya Elimu ya Juu (UDSM, IFM, Tumaini, Mwl. Nyerere) na kasha mjadala wa pamoja,
uliojikita zaidi kwenye uadilifu na hatma ya taifa letu.
Mgeni rasmi
katika siku hii alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa LHRC, Askofu
Mstaafu Elinaza E. Sendoro (aliyewakilishwa na Wakili Fransic Stolla - Rais wa
Chama cha Wanasheria wa Tanganyika), wawakilishi wa Umoja wa Ulaya, Mkurugenzi
Mtendaji wa WiLDAF mama Judith Odunga, Mkurugenzi Mtendaji wa WLAC, na
wawakilishi kutoka mashirika mbalimbali na wanaharakati toka pande mbalimbali
za Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment