Mvua kubwa
iliyonyesha usiku wa leo katika mji wa Iringa imeshusha neema kwa
wakazi wa mji wa Iringa ambao ni wapenzi wa Senene baada ya baadhi
ya wamiliki wa nyumba kudaiwa kuwazuia wapangaji wao kuokota
senene katika nyumba zao huku walimu pamoja na watumishi wa umma
wakichelewa kuingia madarasani kutokana na zoezi la kukamata senene
hao.
Uchunguzi uliofanywa na Francis Godwini(kutoka Iringa) katika shule mbali mbali za
Manispaa ya Iringa asubuhi ya leo umebaini kuwa idadi kubwa ya
wanafunzi na walimu wakia katika mashamba ya shule zao na nje ya
vyumba vya madarasa pamoja na wanafunzi wao wakifukuza senene wakati
katika baadhi ya ofisi wa umma kama TRA na maeneo ya majeshi ya
ulinzi pia wanajeshi walinaswa wakifukuza senene hao.
Wakati wazazi wa wanafunzi hao wakilalamikia hatua ya walimu wa
shule za msingi kuwatumia wanafunzi katika kuokota senene kwa
upande wao baadhi ya wamiliki wa nyumba katika mji wa Iringa
wamedaiwa kuwanyanyasa wapangaji wao kwa kuwazuia kuokota senene
zinazoanguka katika nyumba zao kwa madai kuwa senene hizo ni mali
ya mwenye nyumba na iwapo wanataka basi kutoka nje ya uzio wa nyumba
hizo usiku kwenda kusaka senene mitaani .
|
No comments:
Post a Comment