WAZIRI wa Ujenzi, John Magufuli amemteua
Prof Ninatubu Lema kutoka Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET), kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), uteuzi huo unaanzia
Desemba 20 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya
Magufuli iliyosambazwa kweye vyombo vya habari jijini Dar es Salaam
jana, na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Herbet Mrango, ilieleza
kuwa uteuzi huo, utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu hadi Desemba 20,
2015.
Kwa mujibu wa sheria Na. 15 ya
mwaka 1997 ya mabadiliko madogo ya sehemu ya 3(3) ya kifungu 1(1) (a),
na 1(2), kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 24 ya mwaka 2007, ndiyo
iliyomfanya Waziri afanye uteuzi wa wajumbe wa Bodi hiyo akiwemo
mwenyekiti huyo.
Katika uteuzi huo, Magufuli pia
aliwataja wajumbe wanane wa bodi hiyo ya ERB, kuwa ni pamoja na Fintan
Kilowoko kutoka wizara hiyo, ambapo kwa sasa ni mkurugenzi wa Barabara
za Mikoa, Joseph Malongo, ambaye kwa sasa ni Msajili Msaidizi Huduma za
Usajili na Gemma Modu kutoka Baraza la taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE),
Nuberis Nyange kutoka Chama cha Wahandisi Washauri nchini (ACET).
Wengine ni Sarah Barahamoka,
kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Edwin Ngonyani kutoka
Wizara ya Nishati na Madini, Prof Bakari Mwinyiwiwa; Mhandisi
Mwandamizi, Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET), kutoka Chuo Kikuu
cha Dar es salaam na Prof. John Kandoro; Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia
Dar es Salaam (DIT).
Waziri alisema kuwa jukumu la
msingi la Bodi hiyo ya Usajili wa Wahandisi ni kusajili wahandisi pamoja
na Kampuni zinazotoa ushauri wa kihandisi, kuendeleza wahandisi
kitaaluma, kuwajengea uwezo wa Wahandisi wa kitanzania.
Pamoja na kuandaa nakuchapisha makala mbalimbali yanayohusu shughuli za kihandisi nchini.
No comments:
Post a Comment