Waziri
wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza
kushoto), na Naibu wake Mhe. Stephen Masele wakishiriki katika mkutano
mkuu wa mwaka wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika hivi karibuni
mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Mhe. Stephen
Masele akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa wachimbaji
wadogo wa madini nchini, uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.
Uongozi wa mpito kitaifa wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mara
baada ya kuchaguliwa na mkutano wao mkuu wa mwaka uliofanyika hivi
karibuni mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza
kushoto), na Naibu wake Mhe. Stephen Masele wakishiriki katika mkutano
mkuu wa mwaka wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika hivi karibuni
mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa
Sospeter Muhongo (katikati) katika picha ya pamoja na makamishna
wasaidizi wa madini kutoka kanda mbalimbali, mara baada ya kufunga
mkutano mkuu wa mwaka wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika hivi
karibuni mjini Dodoma.
Wizara ya Nishati na Madini imetenga jumla ya shilingi bilioni 8.9 kwa
dhamira ya kuwainua wachimbaji wadogo wa madini nchini ili kukuza kipato
chao na hivyo kuboresha maisha yao.
Aidha, jitihada za kuwainua wachimbaji wadogo zinalenga pia kuinua pato
la taifa kutokana na kuongezeka kiwango cha kodi na tozo mbalimbali
zinazopaswa kulipwa na wachimbaji hao kwa serikali.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
alipokuwa akizungumza na wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu wa mwaka wa
wachimbaji wadogo wa madini nchini, uliofanyika mjini Dodoma tarehe sita
na saba mwezi huu.
No comments:
Post a Comment