Pages


Photobucket

Thursday, December 13, 2012

CRDB yabisha hodi Burundi, yafungua tawi

 
Picture
Jengo la Benki ya CRDB - Burundi.
Rais wa Burundi Piere Nkurunziza akiwasili katika sherehe za ufunguzi rasmi wa Benki ya CRDB jijini Bujumbura, Burundi. Benki ya CRDB imekuwa Benki ya kwanza ya kizalendo kufungua tawi lake nchini Burundi.

Rais wa Burundi,Mheshimiwa Piere Nkurunziza akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Benki ya CRDB nchini Burundi.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei.

Raisi wa Burundi Mheshimiwa Piere Nkurunziza akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB Tully Esther Mwambapa alipokuwa akiwasili katika sherehe hizo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Burundi Dkt. James Nzagi (Kushoto) na Katibu wa Benki hiyo Bwana John Rugambo (wa pili kushoto) na Meneja Mkuu wa Benki ya CRDB Nchini Burundi Bw. Bruce Mwile.

Raisi wa Burundi Mheshimiwa Piere Nkurunziza akiwa katika ya pamoja na uongozi wa juu wa Benki ya CRDB.

Msanii wa kimataifa kutoka nchini Burundi, Nimbona Jean Pierre “KIDUM” aliburudisha halaiki iliyojitokeza katika uzinduzi.

Nimbona Jean Pierre “KIDUM” 

Hawa pia ni wafanyakazi wa benki ya CRDB Burundi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya uzinduzi.




Wafanyakazi wa Benki ya CRDB nchini Burundi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzano kutoka Dar es Salaam.

Source: http://www.wavuti.com

No comments:

Post a Comment