Jaji mkuu, alitoa maelezo haya jana alipozungumza na gazeti hili katika
mahojiano maalumu kwenye mahafali ya 12 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto (IJA).
JAJI Mkuu, Mohamed Chande Othman, ambaye
amefafanua suala la yeye kutoshiriki katika kesi ya aliyekuwa Mbunge wa
Arusha Godbless Lema Mwananchi
JAJI Mkuu, Mohamed Chande Othman ameeleza sababu za kutokuwa kwenye jopo
la majaji waliopangwa kusikiliza kesi ya aliyekuwa mbunge wa Chadema
mkoani Arusha, Godbless Lema.
Jaji mkuu, alitoa maelezo haya jana alipozungumza na gazeti hili katika
mahojiano maalumu kwenye mahafali ya 12 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto (IJA).
“Ngoja nitolee ufafanuzi suala hilo ili jamii itambue utaratibu wa
uendeshaji wa Mahakama ya Rufani, ambayo ina majaji 16 nchini,” alisema
Jaji Othman.
Jaji Othman alisema kimsingi hajajitoa kushughulikia kesi hiyo, ila siku
ambayo kesi hiyo inatajwa, atakuwa nchini India kuhudhuria Mkutano Mkuu
wa 13 wa Majaji Wakuu Duniani.
Maelezo hayo ya Jaji Chande yamekuja siku tatu baada ya gazeti hili
kuripoti kuwa, mkuu huyo wa mhimili wa Mahakama nchini amejitoa
kusikiliza kesi hiyo na nafasi yake imechukuliwa na Jaji Bernard Luanda.
“Kwanza ifahamike kwamba, jaji wa Mahakama ya rufani hana ubia na kesi
yoyote kwa mujibu wa utaratibu. Jaji yeyote kati ya majaji 16 wa
mahakama ya rufani nchini ana mamlaka ya kusikiliza kesi yoyote ya
rufani,” alieleza Jaji Othman.
Jaji Othman alifafanua kuwa, rufani ya Lema ni miongoni mwa kesi tatu za
uchaguzi zilizobaki ambazo kwa mujibu wa taratibu za kisheria, huanza
kusikilizwa baada ya muda wa mwaka mmoja na hukumu yake ni lazima
itolewe ndani ya mwaka mmoja tangu kuanza kwake.
“Hivyo basi, kwa vile Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufaa anaweza
kuisikiliza kesi hiyo, hakukuwa na sababu inisubiri mimi,” alisema.
Jaji Othman alitaja kesi nyingine za uchaguzi zitakazoanza kufanyiwa
vikao vya rufani na jopo la majaji wa Mahakama ya Rufani kuwa, ni ile ya
Jimbo la Ubungo kati ya Hawa Ng’umbi na John Mnyika ambayo itakuwa
chini ya jopo la majaji watatu; Jaji Nathalia Kimaro, Jaji Salum, Salum
Masati na Jaji Katherine Oriyo.
Nyingine ni ya Jimbo la Ilemela ya Yusuph Yussuph Masengela Lupilya na
wenzake wawili dhidi ya Highness Kiwia na wenzake wawili, ambayo itakuwa
chini ya jopo la Majaji Januari Msofe, Jaji Beard Luanda na Jaji Salum
Massati.
Alisema rufani ya Lema haijaanza kusikilizwa kwa jaji yeyote, hivyo yeye asingeweza kujitoa kwa kuwa hajapangiwa.
“Kinachotatiza hapa ni kwamba, watu wanaifungamanisha rufani hii na ile
ya Arusha ambayo mimi nilikuwa miongoni mwa jopo la majaji kama
mwenyekiti.
Chanzo Mwananchi
No comments:
Post a Comment