Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kufungua kikao cha
dharura cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kwa ajili ya kupokea na
kujadiili taarifa ya uchunguzi wa mgogoro kati ya muwekezaji katika
shamba la malonje ambaye ni Ephata Ministry na wanakijiji wanaolizunguka
shamba hilo wa vijiji vya Malonje, Skaungu naMawenzusi leo katika
ukumbi wa RDC unaomilikiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo. Taarifa hiyo
iliandaliwa na kamati aliyoiunda Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kuchunguza juu ya
sakata hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa kushoto akajadili namna ya kuongoza kikao hicho. Kulia
na Katabu Tawala wa Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima. Mkuu huyo wa
Mkoa alisisitiza kuwa nia na azma yake akiwepo madarakani atajitahidi
kuhakikisha anashughulikia migogoro yote Mkoani Rukwa hata kama matokeo
yake na suluhu yatagusa maslahi ya watu.
Kutoka
kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang’a na Mkuu wa
Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyeka wakifuatilia taarifa katika
kikao hicho.
Baadhi
ya wajumbe halali wa kikao hicho. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Nkasi
Kaskazini Ndugu Ali Kesi, watatu kulia Mbunge wa Jimbo la Kwela Ndugu
Iganas Malocha, Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Ndugu William
Shimwela na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ndugu
Godfrey Sichona.
Wajumbe wa kikao hicho vyombo vya ulinzi na usalama.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akisoma taarifa ya
uchunguzi wa mgogoro wa shamba la Malonje la muwekezaji Ephata Ministry
na wananchi wa vijiji jirani na shamba hilo leo katika ukumbi wa Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa huo(RDC), taarifa hiyo iliwasilishwa na kupokelewa na
wajumbe wa kikao hicho ambacho kwa ujumla waliipongeza kamati iliyoundwa
na Mkuu wa Mkoa huo kuchunguza sakata hilo linaloibua sura mpya katika
vipindi tofauti.
Mshauri wa Kitengo cha Serikali za Mitaa katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa Ndugu Francis Ikayo akichangia katika kikao hicho.
Mratibu
wa mradi wa afya ya mama na mwana kutoka shirika lisilo la kiserikali
la kimataifa la Africare Ndugu Gasper Materu akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa mradi unadhaminiwa na shirika hilo Mkoani Rukwa. Katika
taarifa yake hiyo alisema kuwa jumla ya wahudumu wa afya 2880 katika
ngazi ya jamii wameshapatiwa elimu juu ya mpango wa uzazi salama
kupunguza vifo vya mama na watoto Mkoani Rukwa. Aliongeza kwa kusema
kuwa washiriki wote hao wamewezeshwa baiskeli ili kuweza kuzungukia kaya
mbalimbali katika maeneo yao ili kuwafikishia wananchi wengi zaidi
elimu hiyo.
Baadhi
ya waalikwa katika kikao hicho ambao pia ni wawakilishi wa muwekezaji
Ephata Ministry wakipitia makabrasha ya kikao hicho.
Waalikwa wengine na washiriki wa kikao hicho wakifuatilia msomaji wa taarifa hiyo ya uchunguzi.Picha Na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa-rukwareview.blogspot.com
No comments:
Post a Comment