Pages


Photobucket

Monday, December 31, 2012

DALADALA YAWAKA MOTO IRINGA, ABIRIA WANUSURIKA KUFA



Daladala likizimwa moto na kikosi cha moto Iringa

Daladala yenye namba T 717 AWK mali ya Ayubu Kabigi ikiwaka moto eneo la mshindo.
 
Na: Denis Mlowe - Iringa
Zaidi ya abiria 20 wanusurika kufa katika ajali ya gari aina ya daladala inayofanya shughuli za kusafirisha abiria kati ya Mkwawa na Kihesa Kilolo baada ya daladala hiyo kuungua moto na kuteketea kabisa chanzo kikiwa ni hitilafu katika mfumo wa injini.

Ajali hiyo iliyotokea mida ya saa saba mchana ilihusisha daladala aina ya kipanya yenye namba T 717 AWK mali ya Ayubu Kabigi ilitokea katika maeneo ya Mshindo karibu kabisa na kituo cha mafuta cha Sherry na Kanisa kongwe la Mshindo mkoani hapa.

Shuhuda ya ajali hiyo Anthony Zamilinga amesema kwamba gari hiyo ilikuwa ikitokea maeneo ya Mwangata ilipofika sehemu ya tukio alimwona dereva akishuka na kuanza kuchukua mchanga kwa lengo la kupambana na moto uliokuwa ukianza kuwaka na ulipozidi baadhi ya abiria wakaanza kuruka katika gari hiyo na kupiga simu katika kikosi cha zima moto kilichofika haraka eneo la tukio na kuzima katika gari hilo licha ya kuungua na kuteketea kabisa.
Msemaji wa Zimamoto Kaimu Mkuu wa Kituo Sajenti Meja John Zakaria amesema chanzo cha ajali hiyo hitalafu ya umeme iliyotokea katika gari hiyo na kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwa na tabia ya kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika magari yao. “kikosi cha zimamoto kinatoa elimu kila mara kuhusu elimu ya kukabiliana na majanga ya moto na kuna namba za simu za dharura ambazo ziko wazi wakati wote lakini wananchi hawana tabia ya kutoa taarifa mapema na ndio maana hasara kama hizi zinajitokeza hivyo hatuwezi kuota kama kuna janga la moto hivyo naomba ushirikiano wa wananchi katika majanga ya moto kama haya” alisema Sajenti Meja Zakaria

Mmiliki wa dala dala hiyo Ayubu Kabigi amesema kwamba amepata hasara ya sh milioni 8 kutokana na ajali hiyo na amewashukuru sana wananchi waliojitokeza kusaidia kuzima gari yake kwani wakati anapigiwa simu alikuwa anajiandaa na safari ya nje ya mkoa. “nawashukuru sana wananchi wa maeneo ya mshindo na kikosi cha zimamoto kuwahi kufika mara baada ya kupewa habari kuhusu janga hilo licha ya kwamba gari lilikuwa limewaka moto na kuteketea” alisema Kabigi.

URAIS 2015: CHADEMA SASA VIPANDE VIWILI


SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumtangaza Dk Willibrod Slaa kuwa ndiye mgombea wa urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama hicho, makada wa chama hicho wamegawanyika baadhi wakimponda na wengine kumuunga mkono.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya makada wa chama hicho walisema mwenyekiti wao amekosea kumtangaza mgombea kabla ya wakati, huku wanaomuunga mkono wakisema hajakosea kwa sababu hatua hiyo itasaidia kuondoa makundi ndani ya chama hicho.

Juzi, Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Karatu mkoani Arusha, alisema Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa atapewa fursa ya kuwania tena urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, huku mwenyewe akijiweka kando kuwania nafasi hiyo

Hata hivyo, Dk Slaa alipoulizwa iwapo ana nia ya kuwania nafasi hiyo alihoji: “Kwani mwaka 2010 nilijitangaza mwenyewe,? Iwapo wanachama wa Chadema watanipendekeza nitafikiria kufanya hivyo.” 

Mwasisi wa chama hicho Edwin Mtei, Wajumbe wa Kamati Kuu; Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Bavicha John Heche na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa maoni yanayopingana kuhusu kauli hiyo ya Mbowe.

Wanaounga mkono

“Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama,” alisema Mtei.

Ingawa Mtei hakuwa tayari kusema ni kikao gani kilichopitisha jina la Dk Slaa kuwania nafasi hiyo, alisisitiza: “Kuna vikao vya Kamati Kuu vimefanyika hivi karibuni, vinaweza kuwa vimefanya uamuzi huo. Mwenyekiti hawezi kuzungumza jambo bila baraka za vikao vya chama.”

Hata hivyo, kauli hiyo ya Mtei inapingana na ile aliyoitoa Oktoba 6, mwaka huu baada ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kutangaza kutogombea tena ubunge badala yake kusema anataka kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Mtei alisema hatua ya Zitto kutangaza kuwania urais mapema kungesababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama hicho.

Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.

“Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga.”

Alisema mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015 kumekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema.

Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais huku akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

Hata hivyo, Zitto jana alikataa kuzungumzia suala hilo akisema: “Nimesikia hata mimi kwenye vyombo vya habari ila sina cha kuzungumza kuhusu hilo.”

Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), John Heche alisema kauli hiyo Mbowe siyo yake binafsi, bali ni ya wananchi.

Chanzo: Mwananchi
 

MAZISHI YA MWANAFUNZI WA UDAKTARI ALIYEBAKWA NCHINI INDIA YAFANYIKA








Hatimaye mazishi ya mwanafunzi wa Udaktari aliyefariki jana jumamosi katika hospitali ya Mount Elizabeth nchini Singapore yamefanyika huko India. Juhudi za Madaktari kuokoa maisha yake zilishindikana kutokana na kuathiriwa zaidi na unyama aliofanyiwa na kundi la wanaume sita katikati ya mwezi huu.

Maombolezo nchini India

Mwili wa mwanamke huyo aliyekuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu tayari uliwasili nyumbani mapema leo asubuhi na kupokelewa kwa heshima kubwa ambapo Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh naye alikuwepo katika mapokezi hayo.

Maelfu ya raia nchini India jana jumamosi waliendelea kukusanyika katika mji mkuu New Delhi wakiwa na mishumaa kama ishara ya maombolezo ya kifo cha mwanafunzi huyo aliyebakwa ndani ya basi katikati ya mwezi huu.

Kwa takribani majuma mawili kumekuwa na ghasia kubwa nchini humo waandamanaji wakipinga unyanyasaji dhidi ya wanawake na kutaka adhabu ya kifo itekelezwe kwa wanaotuhumiwa kwa tukio hilo.

Wanaume sita wanaoshikiliwa kwa kufanya unyama huo sasa wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya binti huyo aliyefariki jana asubuhi katika hospitali ya Mount Elizabeth nchini Singapore ambako alipelekwa kwa matibabu zaidi.
 

MAGAZETI YA LEO JUMATATU YA MWISHO DEC 31 2012


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Sunday, December 30, 2012

TASWIRA ZA WASAFIRI UNION STATION WASHINGTON DC LEO


Washington DC Union Station ni kati ya kituo kikuu  jijini  Washington DC, ambapo wasafiri wengi watumia usafiri wa mabasi na treni kutoka majimbo mbali mbali wakitembelea Washington DC hufikia katika kituo hicho kwajina linajulikama Kama  Union Station .

Washington DC tour bus: Wageni kutoka nchi mbali mbali wanapokuja kutembelea jiji la Washington DC hutumia tour bus kwa kutembezwa sehemu mbali mbali za kihistoria katika siku za Holiday.
Wageni kutoka sehemu mbali mbali walio njee ya kituo hicho cha Union StationWashington DC wakisubiri usafiri wa Tour Bus pamoja na Tex kwa jili ya matembezi ya kihistoria.
Baadhi ya wageni waliowasili Washington DC kwaajili ya Holiday ya Mwaka Mpya
Wageni mbali mbali wakiwa njee ya mjengo mkuu wa Washington DC Union Station waliowasili  kwaajili ya Holiday ya Mwaka Mpya
Baadhi ya texi na basi za tour zilifanya kazi kwa ajili ya wageni kutoka sehemu mbali mbali kuja kujionea jiji la Washington DC kwa Holiday
Polisi akiwa katika ulizi mkali njee ya Washington DC katika kituo kikuu cha  Union Station.

Waziri Magufuli amteua Prof Ninatubu Lema kuwa mwenyekiti wa bodi (ERB)


 
WAZIRI wa Ujenzi, John Magufuli amemteua  Prof Ninatubu Lema kutoka Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET), kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), uteuzi huo unaanzia Desemba 20 mwaka huu.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya Magufuli iliyosambazwa kweye vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Herbet Mrango, ilieleza kuwa uteuzi huo, utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu hadi Desemba 20, 2015.
 
Kwa mujibu wa sheria Na. 15 ya mwaka 1997 ya mabadiliko madogo ya sehemu ya 3(3) ya kifungu 1(1) (a), na 1(2), kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 24 ya mwaka 2007, ndiyo iliyomfanya Waziri afanye uteuzi wa wajumbe wa Bodi hiyo akiwemo mwenyekiti huyo.
 
Katika uteuzi huo, Magufuli pia aliwataja wajumbe wanane wa bodi hiyo ya ERB, kuwa ni pamoja na Fintan Kilowoko kutoka wizara hiyo, ambapo kwa sasa ni mkurugenzi wa Barabara za Mikoa, Joseph Malongo, ambaye kwa sasa ni Msajili Msaidizi Huduma za Usajili na Gemma Modu kutoka Baraza la taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Nuberis Nyange kutoka Chama cha Wahandisi Washauri nchini (ACET).
 
Wengine ni Sarah Barahamoka, kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Edwin Ngonyani kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Prof Bakari Mwinyiwiwa; Mhandisi Mwandamizi, Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET), kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Prof. John Kandoro; Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).
 
Waziri alisema kuwa jukumu la msingi la Bodi hiyo ya Usajili wa Wahandisi ni kusajili wahandisi pamoja na Kampuni zinazotoa ushauri wa kihandisi, kuendeleza wahandisi kitaaluma, kuwajengea uwezo wa Wahandisi wa kitanzania.
 
Pamoja na kuandaa nakuchapisha makala mbalimbali yanayohusu shughuli za kihandisi nchini.

HAYA NDIO MAGAZETI YA LEO 30 12 2012,



.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.