MZEE NGURUMO AKIRI KUFUMANIWA NA MKE WA MTU
Maalim Mohamed Gurumo ‘Mzee Gurumo’.
Akizungumza katika mahojiano na Kipindi cha Mkasi kinachorushwa na
Runinga ya East Africa chini ya Mtangazaji, Salama Jabiri mwanzoni mwa
wiki hii, Gurumo alisema miongoni mwa mambo mabaya ambayo hawezi
kuyasahau maishani mwake ni pamoja na hayo.
KUFUMANIWA:
Katika sakata hilo, Gurumo alisema kuwa ilikuwa ni
mwaka 1961 ambapo alikuwa na uhusiano na mke wa mtu ambaye aligoma
kumtaja, ndipo siku moja wakiwa nyumbani kwa mwanamke huyo ‘wakiponda
kirauli’ ghafla walisikia hodi na ndipo mwanamke huyo alipomwambia kuwa
anayegonga mlango ni mumewe.
“Niliogopa sana, ikabidi nijibanze nyuma
ya mlango, alipoingia tu nikatimua mbio kali sana, lakini hakujua kama
ni mimi,” alisema Gurumo.Kuhusu uvutaji wa bangi, Gurumo alikiri
kuwahi kuonja kilevi hicho ujanani mwake ambapo alibainisha kuwa
alishawishiwa na mwimbaji mwenzake maarufu sana kwa wakati huo.
Alisema
siku ambayo alivuta sigara kubwa, alipofika nyumbani baada ya kutengewa
chakula, alimega ugali na kuchovya kwenye maji ya kunawa akidhani ni
mchuzi. “Siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwangu, nilivuta kutokana na
ushawishi, baada ya kufika nyumbani, wakati wa chakula nilimega ugali na
kuchovya kwenye maji ya kunawa, nikasema mbona mchuzi hauna ladha
nzuri, lakini baadaye nilijutia sana,” alisema Gurumo na kuongeza:
“Nimepitia
maisha ambayo si mazuri sana ujanani, lakini yote hayo ni mapito na
imebaki kama historia tu kwangu, namuomba Mungu anisamehe kwa hayo,”
alisema Gurumo.
Chanzo Global Publishers Blog
No comments:
Post a Comment