Pages


Photobucket

Sunday, September 22, 2013

AL SHABAAB WATHIBITISHA KUHUSIKA KATIKA MAUAJI YA KIGAIDI NAIROBI

Baadhi ya majeruhi katika shambulio la kigaidi jijini Nairobi.
-Wadai Kenya ilipuuza onyo lao
 

-Wasema ni kulipiza kisasi kwa Kenya kijihusisha katika vita ya Somalia
-Watu zaidi ya 30 wadaiwa kupoteza maisha wengine wakijeruhiwa

KUNDI la Alshabaab, limethibitisha kuhusika na shambulio la kigaidi lililotokea jana kwenye jengo la ghorofa nne lenye maduka la Westgate jijini Nairobi, nchini Kenya.

Alshabaab kupitia kwa afisa wake mmoja, imethibisha hilo na kueleza kuwa shambulio lilikuwa na kulipiza kisasi baada ya Kenya kujihusisha na vita ya Somalia.

Hali ilivyokuwa ndani ya jengo lililovamiwa na magaidi.
Walioshuhudia tukio hilo wanadai watu waliovalia magwanda yalioonekana kama ya kijeshi huku wengine wakiwa wamefunika nyuso zao walivamia jengo hilo huku wakifyatua risasi.

Maduka hayo ya Westgate hutendelewa sana na matajiri pamoja na wageni kutoka nchi mbalimbali.

Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab imesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waislamu wasio na hatia nchini Somalia, na shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakumba wasomali nchini Somalia.

Taarifa kutoka Ikulu ya nchini Kenya, zinadai kuwa mmoja wa watuhumiwa aliyekamatwa katika tukio hilo  alifariki kutokana na majeraha yake. Magaidi wapatao kumi walivamia jengo la kifahari la Westgate jana mchana la kuwapiga risasi kiholela Wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida.

No comments:

Post a Comment