Dar es Salaam. Mvutano mkali wa kisheria
uliibuka jana Mahakama Kuu baada ya upande wa mashtaka kutaka kuongeza
shahidi wakati wa usikilizwaji wa kesi ya dawa za kulevya inayomkabili
raia wa Kenya, Mwanaidi Ramadhani Mfundo, maarufu kwa jina la Mama Leila
na wenzake saba.
Ubishi mkali ulianza pale Wakili
Mwandamizi wa Serikali, Prosper Mwangamila alipowasilisha ombi la
kuongeza shahidi kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Eva Mamuya
ambaye alizifanyia dawa hizo uchunguzi wa kimaabara.
Mbele ya Jaji Grace Mwakipesile
anayesikiliza kesi hiyo, Mwangamila alisema: “Kwa vile kesi hii inahusu
dawa za kulevya, tunaomba shahidi huyu aweze kupata nafasi ya kutoa
ushahidi wake”.
Mwangamila ambaye anasaidiwa na Wakili
wa Serikali Mwandamizi, Peter Maugo aliongeza kuwa mashahidi wote
watakaofika mahakamani watatoa ushahidi unaohusu dawa alizofunga Mamuya,
hivyo lazima awepo mahakamni kwa ajili ya kuzifungua.
Kwa kuzingatia mazingira hayo, wakili
huyo aliiomba Mahakama hiyo iahirishe kesi hiyo hadi leo, ili waweze
kuwasilisha taarifa ya kumwongeza shahidi huyo katika mashahidi wao, kwa
mujibu wa kifungu cha 289 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai
(CPA).
Hoja hiyo ilisababisha mabishano ya
kisheria pale mawakili wa utetezi wakiongozwa na Yassin Membar
walipopinga ombi kwa maelezo kwamba kifungu hicho kinautaka upande wa
mashtaka kutoa sababu za kuridhisha za kutaka kumwongeza shahidi mpya,
baada ya usikilizwaji wa awali wa kesi katika Mahakama za chini.
Usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo
ulifanywa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Mawakili hao pia waliutaka upande wa mashtaka kuendelea na ushahidi wa
shahidi mwingine waliyekuwa wamemwandaa.
Wakili mwingine wa utetezi, John
Mapinduzi aliomba Mahakama itupilie mbali ombi la Jamhuri, akidai kuwa
linalenga kuwahujumu wateja wao na kwamba ushahidi huo haukuwapo awali,
badala yake unataka kupikwa.
Jaji Mwakipesile baada ya kusikiliza
hoja za pande zote aliahirisha shauri hilo hadi leo kwa ajili ya kutoa
uamuzi wa ombi hilo la upande wa Jamhuri.
Mama Leila ambaye pia hujulikana kwa
majina ya Naima Mohammed Nyakiniwa, anadaiwa kuwa mfanyabiashara wa dawa
za kulevya wa kimataifa ambaye amewahi pia kutajwa na Rais wa Marekani,
Barrack Obama, kuwa ni mtu hatari kwa biashara hiyo.
Katika kesi hiyo yeye na wenzake
wanakabiliwa na shtaka la kuingiza nchini Tanzania dawa za kulevya aina
ya Cocaine, zenye uzito wa kilo 5 ambazo zinadaiwa kuwa na thamani ya
Sh225 milioni.
Washtakiwa wengine Antony Arthur Karanja
na Ben Ngare Macharia (wote Wakenya); na Watanzania watano; Sarah
Munuo, Almas Said, Yahya Ibrahim, Aisha Kungwi, Rajabu Juma Mzome na
John William.

No comments:
Post a Comment