Waziri Mkuu Bw.Mizengo Pinda na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) wameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam , itupilie mbali kesi iliyofunguliwa dhidi yao na Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kuwa kituo hicho hakina haki
kuwafungulia kesi hiyo.
Hoja za Msingi walizozitoa za kuomba kesi hiyo ifutwe ni:
1. Kesi hiyo haipo kisheria na Sheria ya Kinga , Haki na Madaraka ya Bunge;
2. Kesi hiyo inapingana na sheria namba 6
, Kanuni ya 3 ya kesi ya madai pamoja na amri ya 28 na kanuni ya kwanza
ya sheria hiyo;
3. walalamikaji katika kesi hiyo hawana
haki ya kufungua shauri hilo, kuingilia shughuli za Bunge ambapo amri
zinazoombwa na mdai(LHRC), haziwezi kutolewa kwa sababu zinaenda kinyume
na sheria za msingi.
Mahakama imetoa siku 14 kwa LHRC
kuwasilisha majibu ya hoja za pingamizi hilo la awali ambalo
limewasilishwa na AG pamoja na BW. PINDA.
No comments:
Post a Comment