Na Abdi Suleiman, Zanzibar
KATIKA
hali isiyo ya kawaida, kijana Faizi Haji Juma (22), mkazi wa Mchanga wa
Kwale Wilaya ya Chakechake, Pemba aliwashangaza wananchi baada ya
kuwatoroka askari wamemdhibiti ndani ya jengo la mahakama ya
wilaya hiyo.
waliokuwa Kijana
huyo anayekabiliwa na makosa mawili katika mahakama mbili tofauti,
likiwemo la ubakaji na shambulio la mwili kwa lengo la kutaka kubaka,
aliwachomoka askari na kukimbilia baharini katika Soko la Katari.
Baada
ya kukimbia kwa muda, askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba,
Agustino Awe na Koplo Mohamed Hamza, walilazimika kumkimbiza kwenye
matope na kuhakikisha wanamtia mikononi mtuhumiwa huyo na kumrudisha
mahakamani.
Baada ya kurudishwa ndani ya viunga vya mahakama ya
wilaya, mtuhumiwa huyo alitakiwa kuieleza korti sababu zilizomfanya
akimbie lakini akaishia kubabaika.
Hakimu Omar Mcha Hamza alihamaki
baada ya kushuhudia tukio hilo ambapo aliporejeshwa, aliamuru mtuhumiwa
huyo kurudishwa rumande.
“Mdhamini
amekataa dhamana yake leo, mbele ya mahakama hii na tunamfutia dhamana
yake ambayo alitakiwa kuweka ahadi ya maandishi ya shilingi laki moja na
mtuhumiwa kima hichohicho,” alisema hakimu.
Kabla ya kurudishwa
rumande, mdhamini wa mtuhumiwa huyo ambaye ni baba yake mzazi, Haji Juma
aliiomba mahakama kumfutia dhamana juu ya mtuhumiwa huyo na kuiachia
mahakama jukumu hilo, ndipo hakimu alipoamuru kumrejesha tena rumande
hadi Septemba 23, mwaka huu.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa la shambulio la kuumiza mwili kinyume na sheria.
Hati
ya mashtaka iliyowasilishwa mahakamani hapo, ilidai kuwa mnamo Mei 8,
mwaka huu, kati ya saa 10:20 huko Mabonde ya Mpunga Mbuzini, Wilaya ya
Chakechake, Pemba, alimshambulia kwa kisu na kumkata vidole vya mkono
mlalamikaji (jina linahifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali.
No comments:
Post a Comment