Pages


Photobucket

Saturday, September 14, 2013

Marekani yadai kugundua chanjo inayoangamiza VVU

Wanasayansi nchini Marekani wamegundua chanjo ambayo wanaamini itaweza kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa binadamu. Katika majaribio ya chanjo hiyo, wanasayansi hao wameelezea kuwa imeonyesha mafanikio kwa kuangamiza kabisa virusi wanaofanana na VVU kwa nyani. Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limechapisha kwenye tovuti yake kuwa baada ya kubaini hilo sasa wamekusudia kufanya majaribio ya chanjo hiyo kwa binadamu.

No comments:

Post a Comment