Pages


Photobucket

Friday, September 13, 2013

MAPYA YAIBUKA KESI YA PAPAA MSOFE.


 Mfanyabiashara maarufu Marijani Abubakari maarufu kwa jina la Papaa Msofe (50)
 
Upande wa Jamhuri katika kesi ya mauaji inayomkabili Mfanyabiashara maarufu Marijani Abubakari maarufu kwa jina la Papaa Msofe (50), umeiomba Mahakama itupilie mbali ombi lililotolewa na upande wa utetezi kuitaka Mahakama ifute kesi hiyo kwa kuwa upelelezi unachelewa, ni batili na ni kinyume cha sheria.
Ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, mbele ya Hakimu Hellen Riwa, ulidai kuwa Mahakama haina mamlaka kisheria ya kuliondoa shauri hilo, na katika maamuzi itakayofanya Septemba 23 mwaka huu, itupilie mbali maombi hayo ya upande wa utetezi.

Aidha, Jamhuri ilidai uamuzi pekee ambao ungeletwa mahakamani na upande wa utetezi, ni kuwaomba kuliondoa hilo shauri wakati wakisubiri kukamilisha upelelezi kwa sababu wao ndio waliofungua shauri hilo.

Aliongeza na kudai ombi hilo halikuletwa  kinyume na hilo, upande wa utetezi wanataka kuilazimisha Mahakama kuleta ombi la kufutwa kwa kesi kwa kupitia mgongo wake.

Wakili Kweka alidai mahakama haina mamlaka kisheria kushughulikia ombi hilo na ndiyo maana mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote akiwa anasomewa mashtaka yanayomkabili,kwani wenye dhamana ya kusikiliza kesi hiyo ni Mahakama Kuu pekee.

Papaa Msofe na mwenzake Makongoro Nyerere wanakabiliwa na shtaka la mauaji ya mfanyabiashara mwenzao, Onesphory Kituli.
 
Awali Wakili wa utetezi Beatus Malima  aliwasilisha ombi kuitaka Mahakama kuwachia huru wateja wake kwa madai kwamba upelelezi wa shauri hilo unachukua muda mrefu.

Aliiomba Mahakama iwaachie huru washtakiwa hao na pindi upelelezi utakapokamilika kesi iendelee.
Papaa Msofe, anakabiliwa na kosa la mauaji ambalo ni kinyume na  kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.

Inadaiwa kuwa Novemba 6, mwaka 2011 huko Magomeni Mapipa, alimuua Onesphory Kitoli. Msofe aliposomewa shitaka hilo hakutakiwa kujibu lolote  kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment