Pages


Photobucket

Sunday, September 22, 2013

Upinzani wanguruma Dar, muswada wa mabadiliko ya Katiba wapigwa vita

Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe akihutubia katika mkutano uliojumuisha Vyama vya Siasa, Wanaharakati na taasisi za Dini kujadili Suala la Mchakato wa Katiba unaoendelea.
Mnadhimu mkuu wa Kambi ya Upinzani na mbunge wa Iramba Mh Tundu Lissu akihutubia katika mkutano wa Katiba katika Viwanja vya Jangwani Dar es salaam.
Mchungaji Zakaria Kakobe akihutubia katika Mkutano wa Katiba Viwanja vya Jangwani.
Mwanasheria wa Chadema Mh Mabere Marando akihutubia mamia ya wakazi wa Dar es salaam Katika Mkutano wa Katiba.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Azaveli Lwaitama.
Baadhi ya Wafuasi wa Chama Cha wananchi CUF wakisikiliza hotuba katika mkutano wa Katiba ulioandaliwa na Umoja wa Vyama vya Siasa na Wanaharakati uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani.


Mbunge wa Ubungo Mh John Mnyika akihutubia katika Mkutano wa Katiba Ulioitishwa na Umoja wa Vyama vya siasa, Wanaharakati na Viongozi wa Dini.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mh James Mbatia akihutubia wakazi wa Dar es salaam katika Mkutano wa suala la katiba uliofanyika katika viwanja vya Jangwani.
Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam wakisikiliza Viongozi wa Vyama Vya Siasa katika mkutano wa Suala la Katiba uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani.

No comments:

Post a Comment