Pages


Photobucket

Tuesday, January 29, 2013

Waziri Mukangara atembelea Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) jijini dar


Meneja Uchapishaji wa Shirika la Magazeti la Serikali(TSN) John Mcharo(kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara(wa pili kushoto) jinsi wanachapisha magazeti leo jijini Dar es salaam alipowatembelea ili kujionea shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na Shirika la Magazeti ya Serikali. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya TSN Profesa Moses Warioba( wa tatu kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Magazeti ya Serikali(TSN) Gabriel Nderumaki (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (kulia).
Kaimu Mhariri Mteandaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) Gabriel Nderumaki akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara(katikati) jinsi wanavyohariri habari mbalimbali leo jijini Dar es salaam alipowatembelea ili kujionea shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na Shirika la Magazeti ya Serikali.


Kaimu Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti la Serikali (TSN) Gabriel Nderumaki(wa pili kulia) akisisitiza jambo kwa Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara (kushoto) jana leo jijini Dar es salaam alipowatembelea ili kujionea shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na Shirika la Magazeti ya Serikali. Wengini ni Mwenyekiti wa Bodi ya TSN Profesa Moses Warioba( wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene.
Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akijionesha jinsi kurasa za magazeti ya Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) zinavyosanifiwa na wasanifu jana leo jijini Dar es salaam alipowatembelea ili kujionea shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na Shirika la Magazeti ya Serikali.Picha na MAELEZO- Dar es salaam

No comments:

Post a Comment