Pages


Photobucket

Monday, January 28, 2013

WATU 233 WAFARIKI KATIKA UKUMBI WA DENSI BAADA YA KUZUKA MOTO HUKO BRAZIL


 
Zimamoto wakiwakwenye uokoaji katika ukumbi huokatika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria
Watu wakiwa kwenye simanzi katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria
 Uhokoaji ukiendelea  katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria

Raia wa Brazili wanaomboleza vifo vya watu mia mbili thelathini na watatu waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria.Maafisa wanasema kuwa wengi wa waathiriwa walikuwa ni wanafunzi waliokufa baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa .

Wengi wa waliofariki wanaaminika kuwa kati ya miaka 16 na 20
Wengine zaidi ya mia moja wanapata matibabu hospitalini . Serikali ya Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo . Taarifa zinasema kuwa moto huo ulianza wakati waimbaji wa bendi moja walipowasha fataki. Maswali sasa yamekuwa yakiulizwa kuhusu usalama wa kumbui za starehe, huku kukiwa na madai kuwa cheti cha huduma za zima moto kilikuwa kimepitwa na wakati. Hili ni jana kubwa la moto kuwahi kuikumba Brazil kwa zaidi ya miongo mitano Familia za waathiriwa wamekuwa wakiomboleza juu ya majeneza za jamaa zao katika ukumbi wa mamozezi ambao unatuimika kama jumba la kuhifadhia maiti.
Kwa sababu ya heshima kwa waliofariki, serikali iliakhirisha sherehe iliyotarajiwa kufanyika leo Jumatatu katika mji mkuu, Brasilia, kuadhimisha siku 500, kabla ya kombe la dunia kungo'a nagna nchini humo mwaka ujao.
Mazishi ya kwanza mjini Santa Maria yanatarajiwa kufanyika leo , kwa mujibu wa magazeti ya nchi humo. Maafisa wa utawala wametoa majina ya waathiriwa hao,230 huku maiti watatu wakisalia kutotambuliwa. Kulingana na taarifa za kituo cha televisheni cha Globo,wengi wa waathiriwa walikuwa kati ya umri wa miaka16 na 20.
Zaidi ya watu 100 wanapokea matibabu baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.

BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment