Pages


Photobucket

Friday, January 11, 2013

KIJIJI CHA SOMALIA KIKO KATIKA MSHTUKO BAADA YA AL-SHABAAB KUPIGA RISASI KWENYE SHEREHE YA HARUSI

Wakaazi wa Bo'o wamesema wingu jeusi limetanda katika kijiji chao kidogo kutoka washukiwa watatu wa al-Shabaab waliokuwa na silaha kuwapiga risasi wanawake waliokuwa wakitoka kwenye sherehe za harusi wiki iliyopita.

Al-Shabaab imeweka sheria kali kuhusiana na sherehe za harusi ambazo zinajumuisha kupiga marufuku mabibi harusi kutovaa vazi la harusi la utamaduni wa Somalia. [Yasuyoshi Chiba/AFP]

Sherehe hiyo iliadhimishwa kitamaduni kuweka ishara ya siku saba za ndoa na ilihudhuriwa na wanawake tu.

"Ilikuwa siku ya furaha kwa ndugu na rafiki wa maharusi hao, kama inavyopaswa kufanyika wakati kunapokuwa na harusi, na hapakuwa na matatizo [na al-Shabaab hadi shambulio hilo]," alisema Ugas Hirey, mkaazi wa Bo'o mwenye umri wa miaka 35. "Hatuwezi kutambua kilichobadilisha; tulishtushwa na mlio wa risasi na matokeo yake mabaya."

Al-Shabaab wanadhibiti kijiji hicho kilicho kilometa 30 kutoka mji mkuu wa Hiran wa Beledweyne, ambao ulikombolewa na vikosi shirika mwezi Disemba 2011 na kutokea wakati huo wamekuwa wakikataa waziwazi mashambulio kadhaa yaliyofanywa na kikundi hicho kukomboa jiji hilo.

Kwa mujibu wa mzee wa kabila Jama Ahmed mshambuliaji huyo anasadikiwa kuwa na umri kati ya miaka 16 na 19. Alisema walisubiri sherehe hizo kumalizika na kumpiga risasi mwanamke walipokuwa wakiondoka eneo la sherehe, wakamuua shangazi wa bwana harusi na kuwajeruhi wanawake wengine wawili.

Waathirika waliojeruhiwa walikimbizwa mara moja katika Hospitali ya Beledweyne kwa matibabu.

Mmoja wa waathirika alipoteza damu nyingi na alikuwa na hali mbaya sana alipofikishwa hospitali, mkurugenzi wa Hospitali ya Beledweyne Ahmed Khalif aliiambia Sabahi. Wanawake wote wawili kwa sasa hali zao zinaimarika na wanapata matibabu muhimu.

Wakazi wanatii sheria zote za al-Shabaab

Wakazi waliiambia Sabahi walikuwa wanahofia usalama wao na hawaelewi ni kwa nini al-Shabaab walilenga sherehe ya harusi kwa kuwa ilifanyika kwa mujibu wa sheria za wanamgambo. Wengi walikataa kuzungumza kwa kurekodiwa kwa kuhofia ulipizaji kisasi kutoka kikundi cha wanamgambo.

Katika sheria za al-Shabaab, maharusi wanakatazwa kuvaa nguo za utamaduni wa Somalia, gauni jeupe lenye mkono mmoja lililozungushiwa kashida nyekundu na kahawia. Badala yake, wanawake lazima wavae sketi nyeusi ndefu iliyoshonwa kwa kutumia kitambaa kizito na blauzi ndefu inayofunika kuanzia vichwani kwao hadi chini ya kiuno. Zaidi ya hayo, mwanaume na mwanamke lazima watenganishwe, muziki wowote umepigwa marufuku, na msafara wa harusi usiwe na magari zaidi ya matatu.

Mzee wa kabila alisema hakuna mtu aliyekiuka sheria zilizowekwa, na shambulizi halikuwa na sababu kabisa.

Ahmed alisema wakazi wenyeji wanatambua sheria kali ambazo al-Shabaab wameziweka kwa raia kuhusiana na mikusanyiko na sherehe, na kila mtu amekuwa mwangalifu kuzifuata kwa kuwa kikundi cha wanamgambo kinalidhibiti eneo kwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Wageni walighani mkarara ulioitwa "buraanbur" kusherehekea bibi harusi, bwana harusi na familia zao. Mkarara huo haukuhusisha jambo lolote lililozuiliwa na al-Shabaab, alisema.

"Tukio la Bo'o limewabainisha watu wanaoishi katika mkoa wa Hiran na kuwaacha wakishangaa kwa sababu al-Shabaab wameibadilisha siku iliyopaswa kuwa ya kusherehekea na kuwa siku ya majonzi," alisema Ahmed. "Inaonyesha al-Shabaab hawana huruma kwa wale wanaoishi chini ya sheria yao."

Wazee wa kabila kimila walijaribu kusuluhisha ugomvi miongoni mwa wananchi ikiwa ni pamoja na matukio ya vurugu kama hii. Hata hivyo, Ahmed alisema haina maana kushirikishwa katika suala hili kwa sababu wapiganaji wa al-Shabaab hawaheshimu wajibu wa wazee na hawatakuwa wasikivu kama watawafuata.

"Hatuwezi kuwavumilia kuendelea na mambo yao mabaya wanayoyafanya kwa sababu tuna wasiwasi yatasababisha uharibifu zaidi," alisema.

Hii sio mara ya kwanza kwa wanamgambo wa al-Shabaab kushambulia sherehe za harusi. Hivi karibuni, sherehe ya harusi ilishambuliwa mwezi wa Disemba katika kijiji cha Qurod karibu na El Bur, na kuua watu wanne na kuwajeruhi wengine tisa, kwa mujibu wa Hiiraan Online ya Somalia.

Al-Shabaab bado hawajasema lolote kuhusiana na shambulio la harusi ya Bo'o.

No comments:

Post a Comment