Pages


Photobucket

Tuesday, January 8, 2013

VICOBA WAPATA MSAADA KUTOKA KWA MH . LOWASSA


edo b6b75
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amevipatia vukundi saba vya Vikoba vilivyopo Wilayani Monduli,kiasi cha shilingi milioni nane kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao.Lowassa amesema yeye ni mkereketwa mkubwa wa Vikoba huku akisisitiza kuwa ni chachu ya maendeleo na kumkwamua mtanzania kutoka katika umasikini. kila kikundi kimepata shilingi millioni moja ambapo kikundi kilichofanya vizuri kimeongezewa shilingi millioni moja zaidi.Pichani ni Mh. Lowassa akikabidhiwa zawadi na mwenyekiti wa Vikoba Kijiji cha Monduli Juu,Dawson Kaaya wakati viongozi wa vikundi hivyo walipomtembelea nyumbani kwake Monduli.edo1 26244
.Baadhi ya wanavikoba wa Monduli Mjini wakimsikiliza Mh. Lowassa

edo2 eed98
Mmoja wa viongozi wa vikundi vya vikoba Kijiji cha Monduli Mjini akisoma risala mbele ya Mh Lowassa.
edo3 1edf2Mhe Edward Lowassa akipewa zawadi na Bi Arafa Ismaild kutoka katika vikundi vya Vikoba Monduli mjini ambao walikwenda kumtembelea nyumbani kwake. Kushoto kwa Mhe ni Bw. Dawson Kaaya ambaye ni Mwenyekiti wa Vikoba Monduli Mjini.

No comments:

Post a Comment