Pages


Photobucket

Tuesday, January 22, 2013

MAMA SALMA KIKWETE ZIARANI NA RAIS UFARANSA

 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akimkabidhi Bwana Antoine Peigney, jarida lenye kumbukumbu mbalimbali za kazi zinazofanywa na taasisi ya WAMA mara baaba ya kufanya mazungumzo na kiongozi huyo wa Red Cross nchini Ufaransa, jana.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kulia)  akizungumza na Mkurugenzi wa Uendeshaji na Uhusiano wa Kimataifa wa Shirika la Red Cross la Ufaransa Bwana Antoine Peigney (wa pili kushoto) kwenye makao Makuu ya Shirika hilo jijini Paris Ufaransa jana. Mama Salma yuko nchini Ufaransa akiambatana na Rais Kikwete katika ziara rasmi ya siku tatu ya kiserikali,
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Ufaransa mara tu baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzungumza na Watanzania hao kwenye ukumbi wa hoteli ya Le Meurice jijini Paris, jana. Picha na John Lukuwi
**************************

*NI MUHIMU WATOTO WAKAPEWA CHANJO KWA WAKATI


Na Anna Nkinda – Paris
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amesisitiza umuhimu wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kupewa chanjo kwa wakati, chakula chenye virutubisho na kuwafundisha kinamama jinsi ya kuwatunza kwa  kufanya hivyo nchi itakuwa inapanda mbegu nzuri na baada ya miaka michache taifa litakuwa na watoto wenye afya bora.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ameyasema hayo jana wakati akiongea na wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu la nchini Ufaransa ambalo licha ya kutoa huduma mbalimbali za dharula pia linatoa huduma za afya kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema kuwa ili kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano Serikali kwa kushirikiana na shirika la GAVI Alliance kupitia wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ilitoa chanjo ya kuzuia magonjwa ya homa ya vichomi na uti wa mgongo  nchini Tanzania.
“Taasisi ya WAMA imekuwa ikitoa vifaa tiba inavyochangiwa  na wadau  mbalimbali  katika hospitali, vituo vya afya na Zahanati ambazo zimekuwa na upungufu mkubwa wa vifaa hivyo vikiwemo vitanda vya kujifungulia, vitanda vya kulalia wagonjwa, mashine za kupumulia watoto wanaozaliwa wakiwa na matatizo.
Pia kwa kushirikiana na shirika la AMREF International taasisi ya hii imetoa mafunzo kwa  manesi ambao wameweza kuwaelimisha watoto wa kike walioko mashuleni  jinsi ya kujiepusha na mimba za utotoni”, alisema Mama Kikwete.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhusiano na Oparesheni za Kimataifa za Shirika hilo Antoine Peigney alisema kuwa shirika hilo linafanya kazi za kukabiliana na majanga katika nchi 30 Duniani na limeajiri wafanyakazi 17000 pia  watu 20000 kutoka nchi hizo wanafanya kazi za kujitolea.
Alisema kuwa Shirika hilo limekuwa likilisaidia Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania pale lilipoombwa kutoa msaada na kutoa mfano mwaka  2004, 2006 na 2009 lilitoa msaada katika mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam na mwaka 2011 katika mkoa wa Manyara hivyo basi watafurahi zaidi kama watapata nafasi ya kufanya kazi na taasisi ya WAMA ili waweze kuwasaidia watanzania.
Mama Kikwete ameambatana na Mumewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete nchini Ufaransa kwa ajili ya mwaliko wa  ziara ya kiserikali ya siku tatu.

No comments:

Post a Comment