Pages


Photobucket

Wednesday, January 16, 2013

RAIS KIKWETE AMPOKEA MWENYEKITI WA UMOJA WA AFRIKA NA RAIS WA BENIN DKT. BONI YAYI


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akimkaribisha mgeni wake Mheshimiwa Dkt.Boni Yayi wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu julius Nyerere usiku wa jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Dkt.Boni Yayi wakifurahia jambo katika hoteli ya Kilimanjaro jana usiku. Picha na Freddy Maro

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Benin, Mheshimiwa Dkt. Boni Yayi amewasili nchini jana usiku,  Januari 15, 2013, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, Rais Boni Yayi amepokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mara ndege yake ilipotua kiasi cha saa tano na nusu usiku.


Leo asubuhi, viongozi hao wawili watafanya mazungumzo rasmi kabla ya Rais Boni Yayi kuondoka nchini kuendelea na ziara yake Barani Afrika.

No comments:

Post a Comment