Pages


Photobucket

Thursday, January 24, 2013

Gari lachomwa moto Msimbati - Mtwara!! lahusishwa na sakata la gesi



Meza yetu ya habari imepokea taarifa fupi toka Mtwara usiku wa kuamkia leo  ikitujuza kuchomwa moto kwa gari moja linalosadikiwa kutumika kwa biashara ya abiria (TAX)  huko Mtwara. Chanzo chetu kimezidi kunyetisha kuwa mkasa huo unapewa mahusiano na sakata la GESI linaloendelea hivi sasa hapa nchini, kwani gari hiyo inasemekana  lilitaka kumtorosha Bibi mmoja mkazi wa kijiji cha Msimbati - Mtwara aliyetoa ahadi kuwa gesi ikisafirishwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam kama serikali ilivyokusudia basi itageuka  kuwa Maji na si gesi tena! Inasemekana bibi huyo alitaka kwenda kuonana na wazee wa kimila na kuongea na kuhusu suala zima la gesi,  bado haijafahamika nini bibi huyo alitaka kujadili na wazee hao wa kimila.Hadi sasa haijajulikana nani kahusika na tukio hilo na haijajulikana kama kuna watu wameumia kutokana na tukio hilo.
 
Kuwa karibu nasi kwa habari zaidi .............................

No comments:

Post a Comment