Pages


Photobucket

Tuesday, January 1, 2013

UTAWALA WA SOMALILAND KURAHISISHA KANUNI ZA BIASHARA


Utawala wa Somaliland unashughulikia kurahisisha sera zinazoongoza uwekezaji na kuanzisha biashara kama sehemu ya jitihada zake za kuimarisha biashara na kuwavutia wawekezaji wageni na wenyeji.
Wafanyabiashara wakubwa wakionyesha bidhaa zao katika soko la Wahen katika wilaya ya Gaan Libah ya Somaliland. Utawala wa Somaliland inafanyia kazi kurahisisha taratibu za kuanza biashara hapo kwa wajasiriamali. [Barkhad Dahir/Sabahi]

Mwongozo wa Uwekezaji wa Somaliland, umeanzishwa kwa ubia na Wizara ya Biashara na Shirikisho la Biashara la Somaliland, Viwanda na Kilimo, zitakuwa ni mahali pa kutatulia masuala ya uchumi, sheria, mamlaka ya usajiri na taarifa za uwekezaji kwa wenyeji, waliotawanyika kwao na wawekezaji wa kigeni.

"Tutaanzisha tovuti ya kukusanya taarifa kuhusu uwekezaji, fursa zilizopo, mahali pa kuwekeza na taarifa zinazohusiana ili wawekezaji wageni na waliotawanyika kwao na wananchi waweze kupata kwa urahisi taarifa zitakazowasaidia kufanya uamuzi wakati wowote," alisema Mohamed Saleban, mkurugenzi wa mipango na takwimu katika Wizara ya Biashara ya Somaliland.

Tovuti pia itatoa taarifa kuhusu Somaliland, taratibu za kupata leseni, viza zinazohitajika kwa wageni na taarifa zote zinazohusika, alisema.

Kufanyia kazi Mwongozo wa Uwekezaji wa Somaliland ulioanza mwezi Agosti na utakamilika mwezi Januari mwaka 2013, kwa kutumia fedha kutoka Shirika la Marekani kwa ajili ya Maendeleo ya Kimataifa.

Aidha, serikali imeanzisha "eneo moja la biashara" kurahisisha uwekezaji. Jitiahada, zinazofadhiliwa na Benki ya Dunia, zitaanzisha ofisi moja ambayo inaleta pamoja mashirika kadhaa --ikiwa ni pamoja na Wizara ya Biashara, Shirikisho la Biashara, Viwanda na Kilimo, Wizara ya Fedha, na nyinginezo -- kurahisisha mchakato wa kupata leseni na kuwapa wawekezaji taarifa zote wanazozihitaji katika sehemu moja.

Mradi huu, ambao utatekelezwa mwezi Januari, utasaidia wawekezaji kuokoa muda kwa kurahisisha mchakato wa usajiri, alisema.

"Ni fursa nzuri kuepusha vizuizi vyote," alisema Abdirahman Ismail, mkuu wa idara ya mauzo katika Kampuni ya Telesom huko Hargeisa. "Kuwa na eneo moja kwa ajili ya mfumo wa utoaji leseni kutapunguza usumbufu dhidi ya muda unaopotea kujaribu kupata leseni kupitia mawakala mbalimbali."

"Tunakaribisha utekelezaji wake," aliiambia Sabahi. "Utawezesha mtu yeyote anayependa kuanza kwa urahisi kufanya kazi huko Somaliland na kufanya mchakato mrefu ambao mara haukushindika, ambao utaongeza uwezo wa wawekezaji."

Kuondoa vikwazo katika kukua kwa uchumi
Mmiliki wa duka Asha Yusuf, ambaye anauza vifaa vya ujenzi huko Hargeisa, alisema kurahisisha sheria na kufanya taarifa zipatikane zaidi ni hatua katika mwelekeo sahihi, lakini kunahitajika kufanyika zaidi ili kuhimiza wananchi kufungua biashara ndogondogo.

"Hitaji lao la kwanza ni kupata mikopo ambayo inafuata sheria ya kiislamu na sio kutoza faida," alisema.

Baadhi ya benki binafsi zimeanza kutoa mikopo midogo lakini zinahitaji wakopaji kuwa na asilimia 30 ya kiwango cha mkopo kama malipo ya awali, mahitaji ambayo wamiliki wa biashara hawawezi kukamilisha, alisema.

Serikali lazima iweke sera kusaidia biashara kupata fedha kwa ajili ya gharama za kuanzia, alisema. Ni lazima pia itoe miongozo na msaada mwingine unaohitajika ili wamiliki wapya wa biashara wasijisikie upweke katika kufanya biashara kwenye uwekezaji mkubwa.

Saleban alisema Wizara ya Biashara inafanyia kazi programu ya kusaidia utoaji fedha mdogo kwa ajili ya ubia wa umma na binafsi na itaendelea kufanya kazi kuondoa vikwazo vinavyozuia kukua kwa uchumi.

"Lengo [la serikali] ni kuongeza uwekezaji, ambao baadaye utaongeza ajira na kuboresha uchumi wa nchi," alisema. "Mara tutakapopata, kiwango cha ubora wa maisha ya umma kinaweza kuongezeka."

Mabadiliko ya hivi karibuni yalikabiliwa na malalamiko kutoka kwa jamii ya kibiashara na matokeo ya awali kutoka katika utafiti wa Ujasiri wa Biashara wa mwaka 2012 huko Somaliland, ambayo yaliwasilishwa hadharani tarehe 18 Disemba katika Mkutano wa kwanza wa kila mwaka wa Biashara wa Somaliland huko Hargeisa.

Utafiti ulitafuta maoni kutoka kwa wawekezaji na jumuiya ya wafanyabiashara kuhusu mitazamo yao ya mazingira ya biashara Somaliland na vikwazo katika uwekezaji, na ulifanyika Novemba huko Maroodi Jeeh, Awdal, Sahil, Togdheer, Sool na Sanaag.

Utafiti ulipata majibu kutoka kwa wafanyabiashara 273 -- 236 kutoka Somaliland na 37 waliotawanyika kwao -- ukijumuisha wanawake 72.

Utafiti ulionyesha kwamba asilimia 43 ya wahojiwa waliwekeza pungufu ya Dola 10,000 kuanzisha biashara mpya huko Somaliland na asilimia 2.2 tu wamewekeza zaidi ya dola milioni 1.

Uwekezaji ulitiliwa mkazo zaidi huko Maroodi Jeeh, Sahil na Togdheer, ambako zaidi ya asilimia 20 ya biashara zilizotafitiwa ziliwekeza zaidi ya Dola 100,000. Hata hivyo, huko Sool na Awdal, kiasi hicho kilishuka hadi chini ya asilimia 8.

Kwa kuongezea, asilimia 58.5 ya wahojiwa walisema mchakato wa kusajili biashara na kupata leseni ni mgumu, asilimia 43 walisema sheria za kuanzisha biashara zingeweza kuwa na matokeo mazuri katika uamuzi wa uwekezaji wa siku zijazo, wakati asilimia 21 walisema utakuwa na matokeo hasi.

No comments:

Post a Comment