Pages


Photobucket

Wednesday, January 9, 2013

NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI MHE. MWANRI ZIARANI MKOANI RUKWA




Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Aggrey Mwanri akikagua mradi wa maabara katika kituo cha afya cha Matai katika Wilaya mpya ya Kalambo leo. Naibu Waziri huyo amepiga marufuku miradi yote ya serikali hususani inayohusisha mbao kupigwa rangi na badala yake ipakwe vanish, hiyo ni kutokana na baadhi ya wakandarasi kutumia staili hiyo kuiibia Serikali kwa kuweka mbao za bei nafuu na kuzipiga rangi. Mhe. Mwanri yupo Mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku saba ambapo ataembelea halmashauri zote za Mkoa wa Rukwa na kukagua miradi mbalimbali iliyopo chini ya Halmashauri hizo.
Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (kulia) akikagua ujenzi wa banio la mradi wa umwagiliji katika kijiji cha Katuka katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Mhe Mwanri aligoma kuweka jiwe la msingi katika mradi huu kutokana na mkandarasi kujenga mradi huo chini ya kiwango kinyume na mchoro halisi wa mradi huo. Aliagiza mapungufu yarekebishwe ndipo Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a aweke jiwe hilo kwa niaba yake.
Kutoka kushoto ni Mama Mwanri mke wa Naibu Waziri, Mhe. Agrey Mwanri Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Moshi Chang'a Mkuu wa Wilaya ya Kalmabo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Godfrey Schona wakiwa katika picha ya pamoja pembezoni mwa fukwe za Ziwa Tanganyika katika Hoteli ya Liemba Beach Resort walipotembelea ikiwa ni sehemu ya ziara yake Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiweka jiwe la msingi katika nyumba ya mganga wa kituo cha afya Matai mapema hii leo. Katika miradi miwili aliyotembelea Mhe. Mwanri aligoma kuweka mawe ya msingi hadi hapo marekebisho aliyoagiza yatakapofanyiwa kazi ndipo mawe hayo yawekwe kwa niaba yake. 
Naibu Waziri wa TAMISEMI Ndugu Agrey Mwanri akipanda kwa tahadhari kubwa katika daraja la Mto Momba linalounganisha wananchi wa Kilyamatundu Mkoani Rukwa na wale wa Kamsamba Mkaoni Mbeya. Daraja hili lililojengwa kwa kamba limekuwa halikidhi haja ya wananchi hao jambo wanaloomba Serikali kuwajengea daraja litakalowawezesha kuvuka na kuvusha mazao yao kirahisi. Picha/Habari Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

No comments:

Post a Comment