D’Banj alishirikiana na washirika wa Kilimo wa Afrika katika uzinduzi wa
kampeni ya ‘Shiriki Kilimo’ (Do Agric) kwenye kongamano la Umoja wa
Afrika. Kampeni hiyo inalenga kuwasaidia watu zaidi ya milioni 85 barani
Afrika kutoka katika lindi la umasikini kupitia uwekezaji maalumu
katika kilimo na sera za kilimo za Maputo zilizoboreshwa.
D’Banj alikuwa mmoja wa waliozungumza Addis Ababa jana wakati wa
uzinduzi wa kampeni hiyo yenye lengo la kuwahamasisha viongozi wa
kisiasa kutumia sera nzuri zitakazonyanyua uzalishaji, kuongeza kipato
na kuondoa mamilioni ya Waafrika kutoka katika umasikini.
“Nataka Waafrika kufahamu kilimo ni msingi mzuri wa uchumi ambacho
kinatakiwa kutiliwa mkazo na kuleta mabadiliko katika uchumi wa wananchi
na nchi na pia tukitilia mkazo tunaweza kuilisha dunia nzima kwa ujumla
sisi kama Waafrika,” alisema D’Banj.
Kwa upande wake mchezaji wa timu ya Manchester City, Toure alisema
wakati viongozi wengine wa Kiafrika wakitoa kauli zenye nia njema, kwa
sasa ni nchi 8 tu zililizotimiza ahadi zake za kuwekeza 10% ya bajeti za
nchi katika kilimo.
“Kwahiyo ni muhimu kufanya zaidi na kwenda mbele zaidi. Kilimo sio muhimu pekee, pia ni lazima. Kilimo kinalipa,” alisemaToure.
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na asasi mbalimbali za kiraia zikiwemo Pan
African Farmers Association (PAFO), Action Aid International , Acord
International, Oxfam na Alliance for Green Revolution In Africa (AGRA)
mbali na asasi hizo mwanasoka wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure pia
ametia saini kuunga mkono uhamasishaji huo.
Source:Habari leo
No comments:
Post a Comment