Matembezi ya amani siku ya Pasaka wilayani kahama mwaka jana 2014 yaliyosababisha kushuka kwa gharama za matibabu hospitali ya wilaya kikao cha leo. |
Leo tarehe
17/01/2014 Baraza la madiwani wilayani kahama katika kikao chake cha
bajeti limeungana na chama cha NCCR-Mageuzi kwa kukubali mapendekezo ya
kushusha malipo ya hospitali ya wilaya kutoka Shilingi 3000/= mpaka
Shilingi 1000/=. Aidha madiwani hao baada ya kikao waliwaomba viongozi
wa NCCR-Mageuzi hasa katibu aliyekuwa kikaoni hapo kuwa wasisite kuibua
hoja za msingi. Ikumbukwe kuwa mwezi wa pili mwaka jana 2013 Chama cha
NCCR-Mageuzi kilikuwa na ziara ya Opersheni UZALENDO iliyokuwa
ikiongozwa na katibu mwenezi wa vijana Taifa ndugu Deogratius Kisandu
ajenda kuu ilikuwa ni kupunguza gharama za malipo hospitali.
Pia swala hilo liliendelea kuzungumzwa mwezi Desemba
2013 katika uzinduzi wa kitabu cha Utani wa Serikali na Wananchi hapa
wilayani kahama. Leo madiwani wote wa CCM, CHADEMA, CUF na TLP
wameendelea kusema tunakubali changamoto za kila aina na tutaendelea
kuungana na chama cha NCCR-Mageuzi katika hoja zake ili kuboresha wilaya
yetu. hata hivyo Gharama ya sh.1000/= itaanza rasmi tarehe 1/7/2014.
Mytake; AKSANTENI
SANA MADIWANI, MWENYEKITI WA HALMASHAURI, MKURUGENZI NA MKUU WA WILAYA
KWA KUONA UMHIMU WA KUFANYA HIVYO NA MUNGU AWABARIKI SANA. PAMOJA
TUTASHINDA.
No comments:
Post a Comment