Mbeya. Hivi karibuni wananchi wilayani Mbarali
walilalamikia kitendo cha kukodishwa mashamba ya kulima mpunga kwa
masharti magumu yanayotolewa na Mwekezaji wa Kampuni ya Kapunga Rice
Project Limited.
Mwishoni mwa mwaka jana walimweleza Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana kwamba kampuni hiyo inakodi mashamba kwa
masharti magumu ambayo yanamnyonya Mtanzania kwa kiasi kikubwa. Kauli
yao pia ilirudiwa Januari 7, mwaka huu ambapo walimweleza Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwa Kijiji cha Kapunga kwamba
kampuni hiyo imerudisha ubepari nchini.
Aina ya kwanza ya ukodishaji na masharti yake
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kapunga Ramadhan Nyoni
alisema mbinu ya kwanza ya ukodishaji ni ile inayoitwa kilimo cha pamoja
kati ya mkodishaji na mwekezaji.
Utaratibu huu, unahusisha kampuni kutoa huduma za
mbegu ya kupanda, mbolea ya kukuzia DAP, mbolea ya kukuzia UREA na
SA\, mbolea ya kuzalishia MOP, kutengeneza shamba ,kuvuruga, inalipia
gharama ya upandaji, kung’olea magugu, dawa, kupiga dawa na kuvuna.
Mkodishaji yeye kazi yake ni kuhakikisha
anahudumia shamba kwa kutafuta vibarua wa kutosha na kazi inafanyika kwa
muda uliopangwa. Kwa kawaida mwananchi hahitaji mtaji mkubwa kuwekeza
sababu asilimia 97 ya gharama zote inalipwa na kampuni.
Lakini mkataba wake bila kujali ni mpunga kiasi
gani umepatikana katika kila shamba, kampuni inavuna na kuchukua mpunga
kwa ajili ya kujilipa gharama zote ilizozitumia, kulingana na kiwango
ilichokiweka.
Kwa mfano mwaka 2013, kila shamba moja la ekari
15, kampuni inachukua tani 39 au magunia 390 ya mpunga na kwamba mpunga
uliobaki mfano tani saba au magunia 70, kampuni tena ilichukua
asilimia 60 ya mpunga huo na asilimia 40 ya unaobaki alichukua mwanachi.
Nyoni alisema pia kwamba kama shamba husika
litazalisha tani 39 zinazohitajika na kampuni, basi mkulima hawezi
kuambulia chochote kwani kampuni ilichukua magunia yote.
Utaratibu huo ulitajwa kuwa ni mbaya kutokana na
ukweli kwamba haulengi kumsaidia mkulima bali kuinufaisha kampuni kwani
yakitokea mabadiliko ya tabianchi, basi mkulima hawezi kupata hata
mpunga wa chakula.
Aina ya pili ya ukodishaji na adha yake
Utaratibu mwingine wa kukodi shamba uliopo kwenye Kampuni ya Kapunga Rice Project Limited ni ule wa kilimo cha wakulima wa nje.
No comments:
Post a Comment