Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitazama sehemu ya jengo la Kituo cha Polisi cha
kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa ambayo imeporomoka kufuatia
mafuriko yaliyokikumba kijiji hicho kufuatia mvua kubwa zianazoendelea
kunyesha mkoani Dodoma januari 17, 2014. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa
Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua athari za mafuriko yaliyokikumba kijiji
cha Chipogoro wilayani Mpwapwa Januari 17, 2014. Kulia kwake ni Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Mpwapwa, Gregory Tewu na
kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi.
Waziri
Mkuu,Mizengo Pinda akikagua daraja ambalo lilizibwa na maporomoko ya
maji yaliyoambatana na magogo , mawe na udongo na kusababisha mafuriko
katika kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa januari 17,20134.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua athari za mafuriko katika kijiji cha Fufu
wilayani Chamwino, Dodoma, Januari 17, 2014.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Rehema nchimbi na kulia kwake ni Mbunge wa Mtera, Livingstone
Lusinde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda ametembelea vijiji vya Chipogoro na Fufu katika
wilaya za Mpwapwa na Chamwino, mkoani Dodoma na kukagua maeneo
mbalimbali ambayo yaliathiriwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa
zilizonyesha kati ya Januari 2 hadi Januari 11, mwaka huu.
Akiwa
katika kijiji cha Chipogoro tarafa ya Rubi, Waziri Mkuu alikagua kituo
cha polisi na nyumba zilizobomolewa, choo cha zahanati na kukagua eneo
la barabara inayojengwa ya kutoka Dodoma hadi Iringa katika eneo lenye
matatizo ya makaravati kuziba.
Kwenye
kijiji cha Fufu katika tarafa ya Makangwa ambacho kiko umbali wa
kilometa 30 kutoka Chipogoro, Waziri Mkuu alikagua maeneo ya makazi
yaliyoathiriwa kwa mafuriko na kukagua baadhi ya nyumba zilizobomoka
kabla ya kuzungumza na wananchi na kuwapa pole.
Akizungumza
na wakazi wa vijiji hivyo leo (Ijumaa, Januari 17, 2014), mara baada ya
kupokea taarifa za maafa ya mafuriko hayo, Waziri Mkuu alimtaka Meneja
wa TANROADS mkoa wa Dodoma, Eng. Leonard Chimagu kuhakikisha anasimamia
wakandarasi wa barabara hiyo ambayo ujenzi wake bado haujakamilika na
kuainisha maeneo korofi ili yafanyiwe marekebisho haraka.
“Nimekagua
matundu katika daraja moja pale Chipogoro na kuona ni madogo, mtaalamu
anasema uchafu ulioziba ndiyo umesababisha maji yasipite. Mimi si
mhandisi na hizi ni mvua za kwanza tu, sasa yakija maji mengi zaidi ya
haya hali itakuwaje?, alihoji Waziri Mkuu.
“Hata
hapa Fufu, kuna mahali nimeona maji yanaonyesha yalikuja kwa kasi kubwa
lakini upenyo wa kuingia kwenye makaravati na kutokea upande wa pili ni
mdogo sana... barabara hii ni mkombozi lakini kama haitazingatia
uhalisia wa maeneo itakuwa ni balaa,” alionya.
Alimtaka
pia awasimamie wakandarasi hao ili wanapoweka matoleo ya maji
wahakikishe upande wa pili barabara maji hayo yanakwenda kwenye mikondo
ya mto na siyo kuyaacha tu yasambae kiholela na kuishia kwenye makazi ya
watu au mashamba yao.
Waziri
Mkuu aliahidi kutoa mifuko ya saruji 2,600 na mabati 1,560 ambapo kila
kijiji kitapata mifuko 1,300 na mabati 780 ili kuwasaidia wakazi
waliobomolewa nyumba zao waweze kujenga nyumba za kisasa.
Alimwagiza
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi kuwashirikisha wadau wengine
katika mkoa huo ili waone wanawezaje kuchangia upatikanaji wa mabati
mengi zaidi kwa ajili ya nyumba zilizoezuliwa.
Kuhusu
chakula cha msaada, Waziri Mkuu alimtaka Dk. Nchimbi aandae makisio ya
mahitaji ya chakula yaliyopo na kuyafikisha Ofisi ya Waziri Mkuu ambako
kuna Idara inayosimamia maafa ili waletewe chakula hicho haraka kwa
sababu kipo.
Alisema
anakubaliana na ushauri uliotolewa kuhusu suala la ujenzi wa mabwawa ya
kukinga maji ya mvua ili kupunguza kasi ya maji yanayoporomoka kutoka
milimani lakini akasema Serikali imeanza na ujenzi wa Bwawa la Kidete
lililoko wilayani Kilosa tangu yaliyopotokea mafuriko wilayani humo.
No comments:
Post a Comment