Mkuu wa mkoa wa Mara, John Tuppa akielekea kwenye ndege kuongoza
waombolezaji
Rubani wa ndege akielekeza namna ya kutoa
jeneza lenye mwili wa marehemu
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Waumuni wa dini ya kiislamu pamoja na wananchi wa mjini Musoma wakiwa uwanja
wa ndege
Afidh Waziri mmoja wa watu waliotoka na mwili wa Shekh Magee Dar
akiagana na rubani wa ndege
Mwili ukiondoka uwanja wa ndege tayari kupelekwa nyumbani
Msafara wa magari ukisindikiza mwili wa marehemu Shekh Magee nyumbani
Mkuu wa mkoa wa Mara akiwasili nyumbani kwa shekh
Mwili ukishushwa kutoka kwene gari baada ya kufika nyumbani kwake
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu
MKUU wa mkoa wa Mara Mh. John Gabriel Tuppa ameongoza maelfu ya
Wananchi wa Mji wa Musoma kupokea mwili wa Shekh wa Mkoa wa Mara
Athumani Magee aliyefariki dunia usiku wa januari 28 katika hospitali ya
Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Shekh Athumani Magee alifikwa na mauti baada ya kugua kwa muda na mrefu
na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Bugando kwa muda kabla ya
kuhamishiwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi na akiwa njiani kupelekwa
nchini India kwa matibabu zaidi.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliokuwepo kwenye uwanja wa ndege
Musoma wakiusubili mwili wa shekh Magee wamesema wamepata pigo kubwa
kutokana na msiba huo kutokana na Shekh kuwa mstari wa mbele katika
kuhimiza masuala ya dini.
Shekh wa mkoa wa Mara anatarajiwa kuzikwa kesho kabla ya swala ya adhuhur katika makabari ya Musoma Bus mjini Musoma.
INNAH LILLAH WAINNAH ILLAH RAJIUUN
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA SHOMARI BINDA
No comments:
Post a Comment