Pages


Photobucket

Friday, January 31, 2014

JUSTIN BIEBER AJISALIMISHA POLISI NCHINI CANADA KWA KOSA LA KUMSHAMBULIA DEREVA WA LIMO

Bieber mwenye miaka 19 alijisalimisha mwenyewe kwenye kituo cha polisi jijini Toronto ambako alizungukuwa na kundi kubwa la maripota wa TV, wapiga picha na mashabiki wake waliokuwa wakishangilia. Kesi hiyo inakuja ikiwa ni wiki moja baada ya kushikiliwa na polisi kwa kosa jingine huko Miami kwa kuendesha gari akiwa amelewa. Hata hivyo wakili wa muimbaji huyo amesema mteja wake hana hatia.
Polisi jijini Toronto wanasema Justin Bieber alikuwa miongoni mwa watu sita waliochukuliwa na limousine nje ya klabu ya usiku December 30. “Wakati kundi hilo linapelekwa hotelini, ugomvi ulitokea kati ya abiria mmoja na dereva wa limousine hiyo,” maelezo ya polisi yalisema.
Maelezo hayo yamedai wakati wa vurugu huyo, mmoja wao alimpiga dereva nyuma ya kichwa chake mara kadhaa na hivyo limousine kusimama na dereva akaita polisi lakini mtu aliyemshambulia dereva huyo alikimbia.
Kutokana na kosa hilo, Bieber atapanda kizimbani kwenye mahakama ya Toronto, March 10.
Mapema Jumatano hii, jumla ya sahihi 100,000 zilikusanywa kupitia website ya ikulu ya Marekani zinazodai Bieber afukuzwe nchini Marekani. Rais wa Marekani hana mamlaka ya kuagiza kufukuzwa kwa mtu na haijulikani kama White House itajibu malalamiko hayo.

No comments:

Post a Comment