WANACHUO wa Chuo kikuu cha St,Joseph tawi la Songea wamegoma kuingia
madarasani na kutoka kufanya shughuli za aina yeyote ndani ya chuo
hicho huku wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa jumbe mbalimbali
zikiwemo zilizoandikwa wamechoka kunyanyaswa na wakufunzi ambao wengi
wao raia wa India baada ya uongozi wa serikali ya wanachuo kutimuliwa
nyazifa zao na kuwasimamisha masomo kwa muda wa miezi sita.
Kundi la waandishi wa habari wa mjini Songea mara tuu baada ya kupata
taarifa ya tukio hilo walifika kwenye eneo la chuo kikuu cha St,Joseph
kilichopo eneo la Luhuwiko mjini Songea ambako walishuhudia maandamano
makubwa ya wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yaliyo ujumbe mbalimbali
ikiwemo ya wamechoka kunyanyashwa na wakufunzi ambao ni wahindi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Pia wanachuo hao walishuhudiwa wakiimba nyimbo mbalimbali zenye ujumbe
wamechoka kunyanyashwa kwani wao ni watu wazima hapaswi kulinganishwa na
wanafunzi wa shule za msingi au sekondari huku wimbo mwingine ukiwa na
ujumbe kama siyo mwalimu Nyerere kuleta amani wahindi msingefika kwetu
kufanya biashara.
Kufuatia mgomo huo ililazimika askari polisi kufika kwenye eneo hilo
huku wakiwa wamebeba silaha kwa lengo la kutuliza gasia ambao
walitawanywa katika maeneo mbalimbali ya chuo lakini wanachuo
waliendelea na maandamano yao huku wakiimba nyimbo za kushinikiza
uongozi wa chuo uwarejeshe viongozi wa serikali ya wanachuo kwa sababu
ya kutetea haki za wanachuo ambazo walizodai wahidi hao wamekuwa
wakizikiuka.
Wanachuo hao ambao walidai kuwa malalamiko yao walishayafikisha kwa
mkuu wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu wakidai kuwa hali ya mazingira ya
chuo hicho siyo manzuri lakini bado wahindi hao wameendelea na vitendo
viovu licha ya mkuu wa mkoa kuwaangiza kuwa waache kuunyanyasa uongozi
wa serikali ya chuo na wayaweke vizuri mazingira ya chuo hicho ikiwa ni
pamoja na kufanyia matengezo ya vyoo ambavyo vimesababisha baad hi ya
wanachuo kwenda kujisaidia polini.
Walisema kuwa chuo hicho kinavyoo vyenye matundu na wayaweke vizuri
mazingira ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kufanyia matengezo ya vyoo
ambavyo vimesababisha baadhi ya wanachuo kwenda kujisaidia polini.
Walisema kuwa chuo hicho kinavyoo vyenye matundu 14 ambapo kati ya
matundu hayo saba ya wanawake na saba ni wanaume wakati chuo hicho
kinawachuo zaidi ya 1,200 na kufanya kusababisha tundu moja kutumiwa na
wanachuo 64 badala ya kati 20 au 25.
Kwa upande wa viongozi wa serikali ya wanachuo waliyotimuliwa Aristides
Munjwahuzi na waziri mkuu wake Deogratius Sanga waliwaambia waandishi wa
habari kuwa matatizo makubwa yaliyopo ndani ya chuo hicho ni mengi
ambayo wanachuo wakijaribu kulalamika kupitia uongozi wa serikali ya
wanachuo badala yake uongozi wa chuo umefikia kuufukuza uongozi wa
serikali ya chuo na kuwasimamisha masomo kwa muda wa miezi sita jambo
lilionekana kuwa ni uonevu mtupu.
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa chuo hicho mtawa Antonia Emmanuel
alisema kuwa suala la viongozi wa serikali ya wanafunzi la kuvuliwa
madaraka na kusimamishwa masomo walishapewa maelekezo kuwa malalamiko
yao walete kwa maandishi ili yajadiliwe lakini hawakufanya hivyo jambo
ambalo aliliita kuwa ni dharau na badala yake ameshangazwa kuona
wanachuo wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali lakini amesema
tatizo hilo linahitaji kuwepo mazungumzo ya pande zote mbili yakiwa na
lengo la kumaliza tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment