Pages


Photobucket

Monday, January 27, 2014

HALI BADO TETE: UTEKAJI MALORI WASABABISHA MAELFU KUKWAMA NZEGA.


Nzega. Zaidi ya magari 1,000 yamekwama kwenye Barabara Kuu ya Mwanza - Dar es Salaam katika Kijiji cha Ngonho, Kata ya Miguwa, wilayani Nzega, kutokana utekaji wa malori uliofanywa juzi usiku.
Kutokana na tukio hilo, waligoma kuondoa magari yao na kusababisha mabasi ya abiria na malori ya mizigo kukwama wakati abiria wapatao 3,000 wakitaabika kwa kukosa chakula na maji.
Madereva hao waligoma kuondoa magari yao baada ya kukasirishwa na kitendo cha polisi wa Nzega kushindwa kuwasaidia wakati walipotekwa.
Madereva hao wameapa kutoondoa magari hayo hadi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe au Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa watakapofika kwenye eneo hilo ili kusikiliza kilio chao.
Unyama wa watekaji
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nzega, Emmanuel Mihayo alisema watu walijeruhiwa vibaya kwenye utekaji huo kwa kukatwa masikio na kutobolewa macho.


Dk Mihayo aliwataja majeruhi hao kuwa ni raia wa Burundi, Herelina Eddy, ambaye alitobolewa macho na hali yake ilikuwa mbaya na alikuwa kwenye maandalizi ya kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga kwa matibabu zaidi.
Alisema majeruhi wengine wawili wanaendelea vizuri na matibabu katika hospitali hiyo. Majeruhi hao ni Abraham Ismail na Omary Adrian, ambao wote ni wakazi wa Dar es Salaam.
Alisema Adrian alikatwa sikio na shavu pamoja na mkono wa kushoto wakati Ismail alijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili.
Polisi watuhumiwa
Mmoja wa madereva waliotekwa, ambaye aliomba jina lake kuhifadhiwa alisema kuwa polisi wa Nzega waliombwa kutoa msaada lakini walikataa. 

CHANZO MWANANCHI

No comments:

Post a Comment